Alhamisi, 2 Oktoba 2014

SOKWE WABUNI KIFAA CHA KUNYEA MAJI


Watafiti wamegundua kifaa kipya kinachotumiwa na idadi kubwa ya sokwe.

Wanasema kuwa kifaa hicho ni ishara tosha kwamba sokwe wa mwituni wameanzisha tabia mpya.

Wakati kundi la Watafiti hao lilipokuwa likichukua filamu ya sokwe hao katika kituo kimoja nchini Uganda, walibaini kwamba baadhi yao wamekuwa wakitengeneza sponji la majani ambalo hulitumia kunywa maji.

Tabia hiyo mpya tayari imeanza kuenea kwa sokwe wengine.Mtafiti bingwa Catherine Hobaiter kutoka chuo kikuu cha St. Andrews anasema kuwa sokwe hao huliingiza sponji hilo katika vidimbwi vya maji na baadaye kulifyonza.

Ameiambia BBC kwamba waliona vifaa viwili vipya vinavyotumiwa na sokwe hao.

Anasema kuwa alimuona sokwe mwengine akitumia mmea wa Moss badala ya majani kutengeza sponji lake.

Mwengine alichukua sponji lililotumiwa na mwenzake na kuanza kulitumia.

Amesema kuwa ingawaje habari hizo zinaonekana kama zisizokuwa na maana, sokwe hawajakuwa na tabia kama hiyo.BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni