Mahakama
moja nchini Ujerumani imempa idhini mwanamume mmoja kujisaidia haja
ndogo akiwa amesimama baada ya mwenye nyumba kutaka alipwe akidai kuwa
sakafu ya bafu lake iliharibiwa na mkojo wa mpangaji wake.
Mwenye
nyumba ambaye alitaka kulipwa dola 2,200 kwa uharibifu uliofanyika,
alidai kwamba sakafu yake iliyotengezwa kwa mawe aina ya Marble
iliharibiwa na mkojo.Lakini jaji aliamua kwamba njia aliyotumia mwanamume huyo kujisaidia inaambatana na tamaduni nyingi akisema kuwa mtu anapojisaidia akiwa amesimama ni jambo la kaiwada sana.
Kuna mjadala nchini Ujerumani kuhusu ikiwa wanaume wanapaswa kujisaidia haja ndogo wakiwa wanasimama au wakiwa wamekaa kwenye choo.
Baadhi ya vyoo nchini Ujerumani haviwaruhusu watu kujisaidia wakiwa wamesimama, lakini wale wanaoamua kuketi chini huitwa "Sitzpinkler", ikimaanisha kwamba wao sio kama wanaume ni sio jambo la kawaida kwa wanaume kukaa wakiwa wanajisaidia haja ndogo.
Jaji Stefan Hank alikubaliana na ripoti ya wataalamu kwamba tindikali inayotokana na mkojo au Euric Acid, huharibu sakafu nyingi za vyoo.
Lakini kwa kukamilisha amri yake, jaji alisema kwamba wanaume wanaosisitiza kusimama wanapojisaidia haja ndogo, mara kwa mara huvurugana na wenye nyumba lakini hawawezi kuamrishwa kulipa ikiwa sakafu itaharibika
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni