Jumatano, 18 Februari 2015

BOKO HARAM 300 WAUAWA

 
Wanajeshi wa Nigeria wamesema kuwa wamewaua zaidi ya wapiganaji 300 wa kundi la Boko Haram
Jeshi la Nigeria limesema kuwa limewauwa zaidi ya wapiganaji 300 wa Boko Haram, baada ya jeshi la nchi hiyo kutwaa tena miji kadhaa iliyotekwa na wapiganaji hao kaskazini mashariki mwa Monguno.
Msemaji wa jeshi Chris Olukolade amesema kuwa wapiganaji kadhaa wa kiislamu pia wamekamatwa.
Bado hakujatolewa taarifa zaidi kuthibitisha au kukanusha habari hizo.
Mataifa kadhaa ya magharibi mwa Afrika kama vile Niger, Chad na Cameroon, ambayo yanakabiliana na Boko Haram pia yametoa taarifa ya maafa makubwa kwa kundi hilo ambalo limeleta kero kubwa katika ukanda huo.
Siku ya jumatatu wiki hii jeshi la Nigeria lilisema kuwa limeutwaa tena mji wa Monguno, ambao ulikuwa umetekwa na wapiganaji hao wa jihadi mwezi uliopita.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni