Dunia inaadhimisha siku ya Radio. Ni wasaa wa kukumbuka kwamba bila ya
matangazo ya Radio, mamilioni ya watu duniani wasingeliweza kupata
habari sahihi hasa katika maeneo ya migogoro.
Raia wa Jamhuri ya Kidemokarisi ya Congo akisiliza radio katika eneo lenye machafuko Kivu ya Kaskazini
Mfano ni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Kuna msemo
unaosema kwamba ukweli ndiyo unaofyekwa kwanza katika vita. Sababu ni
kwamba watu hawapigani vita kwa kutumia silaha tu, bali pia wanaendesha
propaganda ili kuyaeneza maoni yao.Ni vigumu kupata habari za kweli wakati wa vita. Je vipi radio inaweza kusaidia katika nchi kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Je Radio ina umuhimu gani katika nchi hiyo inayokabiliwa na migogoro mara kwa mara. Hivyo ndivyo matangazo ya radio yanavyosikika katika mji mkuu wa Jamhuri wa Kidemokrasia ya Kongo, Kinshasa, mji wenye wakazi karibu Milioni 10. Watu wengi katika jiji hilo wanaitegemea radio ili kupata habari.
Vipo vituo vya radio zaidi ya 200 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo- maana yake ni kwamba zipo radio zaidi kuliko vituo vya televisheni na magazeti kwa pamoja.
Radio inayoitwa "Digital Kongo" ni mshirika wa DW.
Radio hiyo inatangaza kila siku, kutokea mjini Kinshasa, kwa mamilioni ya wasikilizaji wake .
Mkurugenzi Mkuu wa kituo hicho cha Radio, Severin Bamany amesema "Radio hii bado inasikilizwa na watu wengi wa Kongo. Bado inaendelea kuongoza katika mandhari ya vyombo vya habari vya hapa nchini"
Radio ni njia muhimu ya kupatia habari za ulimwengu na za ndani ya nchi, hasa kwa watu wasiojua kusoma au wale wasiokuwa na uwezo kununua televisheni.
Mwanzoni mwa miaka ya 2000 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilikuwamo katika mvutano mkubwa sana wa kisiasa.
Majeshi ya serikali yalipambana na waasi, mashariki, magharibi na kaskazini, kupigania mamlaka. Mshauri wa masuala ya Radio David Smith anakumbuka kwamba kila jimbo lilikuwa na Radio yake ya kuendeshea propaganda ya kueneza chuki na habari za kupotosha.
Jawabu la tatizo hilo lilipatikana baada ya kuanzishwa Radio Okapi mnamo mwaka wa 2002. Lengo la Radio hiyo iliyoanzishwa kwa msaada Umoja wa Mataifa ni kutangaza habari sahihi nchini Kongo kote.
Ndiyo sababu ilijenga vituo katika miji ya Goma, Bukavu na Kisangani, Na kutokea mji mkuu, Kinshasa radio hiyo inatangaza katika lugha tano za taifa na kutoa habari sahihi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni