Jumapili, 22 Februari 2015

FLOYD MAYWEATHER KUPAMBANA NA PACQUIAO



Floyd Mayweather 

Pambano la pesa nyingi katika historia liko mbioni, Mayweather ameonyesha kopi ya mkataba uliosainiwa pamoja na Manny Pacquiao katika mitandao ya kijamii. 

 

Mpambano huo uliokuwa katika matayarisho kwa muda wa miaka mitano utafanyika MGM Grand Las Vegas. 

 

Wapiganaji wote wawili wana rekodi zinazofanana kwa sababu wote hawajawahi kupigwa katika mapambano yao yote.

 

Utakuwa ni mpambano ghali zaidi kutokea katika historia za ngumi za kulipwa, utagharimu jumla ya Dola za Kimarekani 250. Katika pesa hizo inaeleweka kuwa Mayweather anauhakika wa kuchukuwa Dola milioni 150 wakati Manny Pacquiao atachukuwa dola za kimarekani milioni 100. 

 

Sikuzote Mayweather amekuwa mpiganaji mkubwa katika mikataba yake yote anayoingia kupelekea yeye kupewa kile anachokitaka.

Nakala ya mkataba aliyoonyesha Mayweather kwenye mitandao ya kijamii
Ameweka picha hiyo ya mkataba pamoja na maneno yanayosomeka: “Kile Dunia ilikuwa inasubiria kimeshafika. Floyd Mayweather v/s Manny Pacquiao ni Mei 2, 2015, hili ni dili lililokamilika. Niliwahakikishia masabiki kufanikisha swala hili na tumefanya hivyo. Tutatengeneza historia siku ya Mei 2, Usiache kuja. Huu ni mkataba uliosainiwa na sisi sote."
Kutoka ripoti mbali mbali, vyumba vyote Ndani ya MGM Grand vimechukuliwa ndani ya dakika 3, toka mpambano utangazwe.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni