Jumapili, 22 Februari 2015

MAN U HOI, ARSENAL YAPETA CHELSEA SARE

 

Baadhi ya wachezaji wa Manchester United wakihuzunika baada ya kufungwa
Man United ikiwa ugenini katika uwanja Libert imekubali kupata kichapo toka kwa Swansea kwa kuchapwa bao 2-1.
Anders Herrera alianza kuifungia timu ya la Dakika ya 28 na Swansea kusawazisha Dakika ya 30 kwa Bao la Ki Sung-yueng na kisha Gomis kuwapa ushindi wenyeji.

Vinara wa ligi Chelsea, wakicheza kwao Stamford Bridge, wametoka Sare 1-1 na Burnley ambayo inapigana isishushwe Daraja.
Chelsea walitangulia kufunga kwa Bao la Branislav Ivanovic la Dakika ya 14 lakini wakawa pungufu katika Dakika ya 70 pale Nemanja Matic alipopewa Kadi Nyekundu alipolipizia Rafu toka kwa Ashley Barnes. Burnley walisawazisha kwa Bao la Kichwa la Ben Mee kufuatia Kona ya Dakika ya 81.
Arsenal wakiwa Ugenini walipata ushindi wa Bao 2-1 walipoichapa Crystal Palace na kutwaa Nafasi ya 3 kwa kuishusha Man United Nafasi ya 4. Mabao yakifugwa na Santi Carzola kwa mkwaju wa penati na Giroud.
Bao pekee la Palace lilifungwa Dakika ya 90 na GlennMurray.
Matokeo ya michezo mingine ni kama ifuatavyo:
Aston Villa 1 - 2 Stoke
Hull City 2 - 1 QPR
Sunderland 0 - 0 West Bromwich
Man City 5 - 0 Newcastle

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni