Luis Suarez akifunga bao
Barcelona
imefanikiwa kushinda kwa mabao 2-1 katika mechi ya kwanza ya Ligi ya
Mabingwa hatua ya 16 Bora. Barcelona imeshinda kwa mabao hayo ugenini
dhidi ya wenyeji wake Manchester City huku Luis Suarez akiwa shujaa kwa
kufunga mabao yote mawili. Lionel Messi alipata nafasi ya kufunga mkwaju
wa penalti baada ya kuangushwa na Zabaleta katika dakika ya 90 lakini
Joe Hart akaokoa, mpira ukamrudia Messi, akakosa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni