Carlos Tevez ameendelea kuwa mtamu zaidi ya Mcharo baada ya kuingoza
Juventus kupata ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ya kwanza ya Ligi ya
Mabingwa hatua ya 16 Bora.
Tevez ndiye alifunga bao la kwanza huku Alvaro Morata akitupia la pili.
Marco Reus alifunga bao pekee la Dortmund waliokuwa ugenini hivyo
kufanya mabao yote ya mechi hiyo kuwa yamefungwa katika kipindi cha
kwanza.
Tevez alikuwa mwiba kwa mabeki wa Dortmund, hata hivyo walijitahidi kuhakikisha hawafungwi mabao mengi zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni