WANANCHI
wenye hasira mjini Ilula, mkoani Iringa, wamevamia kituo cha polisi na
kuvunja milango kisha kuwafungulia mahabusu waliokuwemo ndani, wakachoma
moto baadhi ya magari yaliyokuwepo kituoni hapo pamoja na mafaili.
Kwa
mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, tukio hilo limetokea leo asubuhi
kufuatia mwanamke mmoja ambaye hakufahamika jina lake kujigonga ukutani na
kuanguka kisha kufariki dunia wakati akiwakimbia polisi waliokuwa kwenye
oparesheni ya kuwakamata watu wanaokunywa pombe wakati wa asubuhi.
Habari
zaidi zinapasha kwamba, licha ya kuchoma moto magari, waliziba barabara
kuu ya kwenda mikoani na kuyazuia magari kupita, hali iliyosababisha
polisi kuwakabili lakini walizidiwa nguvu na kuingia ndani ya basi la
Nyagawa.
Askari wakiwa ndani ya gari hilo waliendelea kushambuliwa na wananchi kwa mawe na kuvunja vioo vyake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni