Hii si
poa! Raia wenye hasira, katikati ya wiki iliyopita waliwachukua vijana
wawili wanaotuhumiwa kuwa majambazi, waliokuwa mikononi mwa polisi,
ambao majina yao yametajwa kuwa ni Mnubi na White kisha kuwateketeza kwa
moto baada ya kuwabaini kuwa ndiyo waliohusika na uvamizi na uporaji wa
maduka mawili ya huko Mwika-Madukani, Moshi vijijini.
Kesho
yake walikamatwa na wananchi walioshirikiana na polisi, baadaye
kukatokea kutoelewana baada ya jeshi hilo kutaka kuwachukua ili
kuwapeleka mbele ya sheria.
“Polisi
waliwaweka katika gari lao ili waondoke nao, lakini wananchi
waliwachomoa na kuwapa kipigo kisha kuwateketeza kwa moto, askari
walijaribu hata mabomu ya kutoa machozi, lakini wakazidiwa,” kilisema
chanzo hicho.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Godfrey Kamweli alikiri kutokea kwa tukio hilo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni