Rais
wa Afrika kusini Jacob Zuma ameahirisha ziara yake ya ughaibuni
kutokana na hali ya ghasia za kibaguzi dhidi ya wageni katika taifa
lake.
Alitarajiwa kuhudhuria mkutano nchini Indonesia. Rais Zuma
ambaye amekosolewa kwa kushindwa kuonyesha uongozi anatarajiwa
kuitembelea kambi ya wakimbizi ya Chatsworth mjini Durban.Polisi nchini Afrika Kusini wamewaagiza raia kutotuma ujumbe usiothibitishwa kuhusu mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni kwa sababu hatua hiyo inazua hofu.
Polisi wamesema kuwa kuna wasiwasi kuwa uvumi huo unachochea ghasia dhidi ya wahamiaji.
Watu 30 walikamatwa wakati wa ghasia za usiku kucha mjini Johannesburg.
Biashara kadha zinazomilikiwa na raia wa kigeni ziliharibiwa.
Takriban watu watano wameuawa kwenye mashambulizi yaliyoanza baada mfalme wa kizulu Goodwill Zwelethini kusema kuwa wageni wanahitajka kuondoka Afrika Kusini
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni