……………………………………………………………….
Mwandishi Wetu,
Mbunge
wa Vunjo, Augustine Mrema ametangaza mkakati wa kuisambaratisha
NCCR-Mageuzi Vunjo kwa kuzindua rasmi kampeni inayoitwa ‘TOKOMEZA MBATIA
VUNJO’.
Akizungumza
wakati wa mkutano na wanachama wa chama hicho katika Kata ya Makuyuni
Himo, kitongoji cha Kiriche, juzi, Mrema alisema operesheni hiyo ina
lengo la kuhakikisha jitihada za Mbatia kulitwaa Jimbo hilo
hazifanikiwi.
Mrema
ambaye alisema operesheni hiyo ni majibu kwa Mbatia ya kauli yake
ambaye alitangaza ‘Delete TLP/ Mrema’, alisema mwanasiasa mwenzake huyo
anatumia propaganda chafu dhidi yake ikiwa ni pamoja na kudai kazeeka,
hafai na hana uwezo wa kuwaongoza Vunjo.
“Mimi
kuanza sasa natangaza ‘TOKOMEZA MBATIA VUNJO’ na ninasema nipo fiti,
hafi mtu hapa na nina uwezo ninao wa kuendelea kuwaongoza Vunjo kwani
nina mtaji wa kutosha wa watu” alisema.
Mrema
aliitangaza operesheni hiyo muda mfupi baada ya kuwakabidhi kadi
viongozi sita wa NCCR Mageuzi wa Kitongoji cha Kiriche akiwemo
Mwenyekiti wa chama hicho Kata ya Makuyuni, Badi Mandari na wengine 50
kutoka vyama tofauti.
Mbunge
huyo alisema kuwa wakati wa kujua mbivu na mbichi ni sasa na kubainisha
kuwa kuna wanachama wa TLP ambao walirubuniwa na Mbatia lakini baada ya
kuujua ukweli wamerudi katika chama chake.
Mrema
ambaye pia alimkabidhi makalavati manne kwa ajili ya ujenzi wa daraja
katika kitongoji cha Kiriche, alisema mfuko wa Jimbo hadi sasa umetumia
jumla ya shilingi milioni 15.1 kwa ajili ya shughuli za maendeleo katika
Kata hiyo.
Mara
baada ya kupokea makalavati hayo, Mandari, alisema wananchi wa eneo
hilo vipindi vya mvua wamekuwa wakipata adha kubwa ambayo wakati
mwingine imekuwa ikiwafanya wakakosa mawasiliano ya barabara na wenzao
wa maeneo vijiji vingine.
Katika
hatua nyingine, Mrema alikataa kuwasamehe mbele ya mkutano huo madiwani
wawili waliofukuzwa katika chama hicho, Yolanda Lyimo wa Kata ya Kilema
Kati na Meja Jesse Makundi wa Mwika Kaskazini.
“Nimesikia
maombi yenu ya msamaha, lakini katika chama sikuwafukuza mimi Mrema,
bali ni vikao vya chama hivyo suala lenu nalipeleka mbele ya Kamati Kuu
lakini akawashauri ili Kamati Kuu iweze kusikiliza maombi yao sharti
muondoe kesi mnayodai fidia dhidi yangu na Naibu Katibu Mkuu, Nancy
Mrikaria ya shillingi millioni 500” alisema Mrema
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni