Jumatano, 13 Mei 2015

BARCELONA HIYOOOO FAINALI

Messi,Suarez na Naymar wakishangilia bao
Miamba ya soka ya Hispania Barcelona, wamefanikiwa kutinga fainali baada ya kuibwaga Bayern Munich kwa jumla ya mabao 5-3 yaliyopatikana katika mikondo yote miwili waliyokutana kwenye hatua ya nusu fainali.
Katika mchezo wa usiku wa kuamkia leo ambao ulipigwa ndani ya dimba la Allinza Arena, Bayern walipaswa kushinda goli nne bila ili kupata tiketi ya kusonga mbele. Lakini mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa the Bavarian 3, Barcelona 2.
Leo usiku kutakuwa na mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya Juventus kwenye dimba la Benabeu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni