Jumapili, 31 Mei 2015

MAANDAMANO MAKUBWA YAFANYIKA VENEZUELA

 
Waandamanaji Venezuela 
 
Maelfu ya watu wamefanya maandamano ya amani nchini Venezuela wakipitia barabara za mji mkuu Caracas wakitaka kuachiliwa kwa viongozi wa upinzani ambao wamekuwa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Wanasiasa hao ni pamoja na mameya wawili wa zamani Leopoldo Lopez na Daniel Ceballos ambao wanazuiliwa kwa mashtaka ya kuchochea maandamano ya kuipinga serikali.

Rais wa Venezuela Nicholas Maduro amewalaumu kwa vifo 43 vilivyotokea wakati huo.

Wiki hii viongozi hao wa zamani wa upinzani walitangaza kuanza mgomo wa kutokula wakiwa gerezani

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni