Jumanne, 30 Juni 2015

HUKUMU YA MRAMBA, MGONJA NA YONA YAPIGWA KALENDA HADI TAREHE 3/7

  Baadhi ya wasikilizaji wa kesi hiyo wakiwa kwenye chumba maalum kabla ya kuingia mahakamani.
Ndugu wa Mgonja wakiteta jambo.

Mgonja akiwafuatiwa na Mramba kwa nyuma wakitoka mahakamani muda mfupi baada ya kesi hiyo kuahirishwa.
...Wakielekea nje.
....Safari  ya kuondoka mahakama ikiendelea.
Mramba akiwa na mmoja wa mawakili wake.
Mramba na Mgonja wakiteta.  Vigogo hao na baadhi ya wahudhuriaji wakiondoka eneo la mahakama.       Salaamu na mazungumzo ya hapa na pale vilitawala. Mramba akizungumza na ndugu, jamaa na marafiki kabla ya kuondoka.
HUKUMU ya kesi inayowakabili vigogo watatu, aliyekuwa waziri wa fedha, Basil Mramba; aliyekuwa waziri wa nishati na madini, Daniel Yona na aliyekuwa katibu mkuu wizara hiyo, Aggrey Mgonja; iliyokuwa itolewe leo Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam, imeahirishwa kutokana na kukosekana kwa mmoja wa majaji ambaye yuko  Dodoma bungeni.
Mmoja wa majaji aliyekuwa katika ofisi ya hakimu mkazi, John Utamwa, alisema hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa Julai 3, mwaka huu saa saba mchana

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni