Maafisa
wa kijeshi nchini Indonesia, wanasema kwamba ndege ya uchukuzi ya jeshi
la angani la nchi hiyo imeanguka kaskazini mwa jimbo la Sumatra.
Wanasema kuwa tayari miili 20 zimepatikana katika eneo la ajali.Maafisa wa kijeshi nchini Indonesia, wanasema kwamba ndege hiyo ya uchukuzi ya majeshi ya taifa hilo, ilianguka muda mfupi baada ya kupaa angani.
Kuna ripoti kuwa watu bado wanasikika wakipiga mayowe katika majengo yaliyoanguka.
Picha za runinga na kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha moto unatoka kwenye mabaki ya ndege hiyo.
Msemaji wa jeshi la angani alisema kuwa rubani alikuwa ameomba kurejea katika uwanja wa kambi ya kijeshi kwa sababu ya matatizo ya kimitambo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni