Umoja
wa mataifa unasema kuwa Wajeshi wa Sudan Kusini wamewabaka kwa zamu
wasichana wengi kisha wakawachoma moto wakiwa majumbani mwao.
Kwa
mujibu wa ripoti hiyo mpya ya umoja wa mataifa ukatili huo ulitokea
katika eneo la Greater Upper Nile ambako kumekuwa na mapigano makali
kati ya vikosi vya serikali na waasi.Katika tukio moja, mwanamke mmoja alilazimishwa kushika makaa ya moto huku akipigwa katika jaribio la kumshinikiza kutambua waliko waasi.
Umoja wa mataifa vile vile umelaumu pande zote hasimu kwa kuwalazimisha watoto kuwa wanajeshi, ubakaji na mauaji.
Kufikia sasa hakuna upande uliojibu madai hayo dhidi yao
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni