Jumamosi, 13 Juni 2015

WAHAMIAJI NI MUHIMU - UJERUMANI

Wahamiaji haramu wakiwa kwenye mashua
Maafisa nchini Ujerumani wanasema kuwa idadi inayozidi kuongezeka ya wakimbizi wanaowasili kutoka nchi mbalimbali kama Syria watasaidia kujaza pengo la ukosefu wa wataalamu.


Mwenyekiti shirika la ajira nchini Ujerumani aliliambia gazeti moja kuwa watu wanaokimbia Syria, wengine wameelimika na hivyo wanakaribishwa nchini Ujerumani.

Wakimbizi 350,000 watarajiwa kutafuta ajira nchini ujerumani mwaka huu. Ujerumani hupokea maombi mengi ya hifadhi kuliko nchi yoyote katika muungano wa ulaya na idadi hiyo inazidi kuongezeka.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni