Jumatatu, 27 Julai 2015

ABIRIA ATEMBEZA KISU NDANI YA DALADALA NAYE AUAWA

 
Mmoja wa abiria aliyejeruhiwa kwa kisu
Mtu mmoja aliyekuwa abiria ndani ya daladala lililokuwa likitoka mjini kuelekea Makumbusho amewashambulia kwa kisu abiria kadhaa ndani ya gari maeneo ya Magomeni na kuwasababishia majeraha makubwa
 
Majeruhi wote wamekimbizwa hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala.
 
 Mshambuliaji huyo ameuawa na wananchi wenye hasira. 
 
Hadi sasa haijafahamika nini lililkuwa lengo la mshambuliaji huyo.
 
Wananchi wanaendelea kukumbushwa juu ya kutojichukulia sheria mkononi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni