King Nahh
MTOTO
mwenye kipawa cha ajabu katika kutoa ushauri wa kujijengea uwezo wa
kujiamini anayezidi kujipatia umaarufu mkubwa duniani, Lonnie Hudson
maarufu kama ‘King Nahh’(Pichani), ametua jijini Dar es Salaam.
King
Nahh aliambatana na baba yake mzazi , Nyeeam Hudson ambapo wapo nchini
kwa mwaliko wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Wisdom Partners.
Leo
mtoto huyo atafanya kongamano kubwa la watoto na wazazi katika
Ukumbi wa Urafiki ambapo nia na madhumuni ni kuamsha hisia za watu
ambao wamekata tamaa katika masuala mbalimbali na kukosa kujiamini
katika maamuzi.
“Najisikia
furaha kuja Tanzania. Ninaamini nina jukumu kubwa la kufanya hapa.
Hususani kwa watoto ambao bado hawaamini kuwa wanaweza kubadili hisia
zao, kujiamini na kushiriki katika masuala mazima ya maendeleo,”
alisema.
King
Nahh aliongeza kwamba, hisia za watu wengi hivi sasa zimelemaa kutokana
na kuishia kulaumu matatizo na vikwazo bila kutafuta suluhu ya
matatizo yao.
“Kila
mtu analaumu. Wa kwanza atalaumu wa pili, wa tatu, wa nne, wa tano
mpaka wa sita. Wote wanaishia kulaumu jambo moja. Wengine wanaamini kuwa
hawezi kitu. Ila ukweli ni kwamba pale unapokuwa huwezi kitu kuna kitu
unaweza kufanya. Jamii ibadilike. Iache kulaumu,”alisema mtoto huyo na
kushangaza watu waliokwenda kumlaki.
Mkurugenzi
wa taasisi ya Wisdom Partners, Cynthia Henjewelle, alisema kuwa dhamira
kubwa ya kumleta mtoto huyo nchini ni kusaidia kubadili hisia za jamii
hasa watoto ili waweze kujiona kuwa sehemu ya jamii.
“King
Nahh ni miongoni mwa watoto wanaosifika hivi sasa duniani kutokana na
kipawa alichonacho. Wazazi wawalete watoto Urafiki, ili waweze
kubadilishana mawazo. Pia wazazi wanakaribishwa kumsikiliza mtoto huyu
kuanzia saa tano asubuhi,” alieleza Henjewele.
King Nahh akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo
Akikabidhiwa shada la maua uwanjani hapo
King Nahh akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi baada ya kuwasili uwanjani hapo
Meneja wa King Nahh akisisitiza jambo kwa wanahabari
King Nahh akicheza ngoma ya utamaduni
King Nahh akizungumza na wananchi katika viunga vya uwanja wa ndege
Akiwa amepozi na wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo
Akisaini kitabu cha wageni katika Supermarket ya Uchumi
Akimlisha keki mmoja kati ya wafanyakazi wa Uchumi Supermarket
Akilishwa keki na msanii nyota wa filamu, Iluminata Alfonce 'Dotnata'
Akikabidhiwa
'token' na Meneja wa Uchumi Supermarket kwa ajili ya kununulia bidhaa
katika kipindi atakachokuwa nchi, pembeni yake ni mratibu wa kongamano
Cynthia Henjewelle
Akitaniana na wafanyakazi wa Uchumi Supermarket
Akijichagulia bidhaa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni