Jumatatu, 27 Julai 2015

OBAMA AIONYA ETHIOPIA KUHUSU UVUNJIFU WA HAKI ZA BANADAMU

Rais wa Marekani Barak Obama
Rais Obama katika ziara yake ya kwanza ya rais wa Marekani nchini Ethiopia amelionya taifa hilo kwamba linahitaji kuimarisha haki zake za kibinaadamu pamoja na uongozi bora.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari, Barrack Obama amesema kuwa amefanya mazungumzo ya kufana na waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn na kwamba taifa hilo litakuwa thabiti wakati sauti zote zitakaposikika.

Bwana Desalegn amesema kuwa taifa hilo liko katika harakati ya kuweka demokrasia.

Vilevile Obama aliunga mkono maendeleo yaliyoafikiwa na Ethiopia kiuchumi pamoja na usalama wa kieneo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni