Bobbi
Kristina Brown, mtoto wa marehemu Whitney Houston ambaye alikuwa gwiji
wa muziki wa R&B, amefariki dunia baada ya kupoteza fahamu kwa muda
wa miezi sita tangu alipokutwa taabani kwenye bafu lake na alipofikishwa hospitalini na kukutwa na matatizo kwenye ubongo.
Msemaji wa familia Kristen Foster amesema Bobbi amefariki akiwa amezungukwa na familia yake ,''hatimaye yuko salama sasa kwenye mikono ya Mwenyezi Mungu, tunawashukuru wote walioungana nasi katika maombi na kuonesha upendo kwa miezi michache iliyopita''.
Bobbi ambaye alikuwa amepoteza fahamu tangu akutwe ameanguka kwenye bafu lake panapo tarehe 31 Januari mwaka huu na kuwekwa kwenye matibabu huku akiwa amekosa ufahamu na mpaka kifo chake kumkuta alikuwa hajapata fahamu bado. Inakumbukwa kuwa miaka mitatu iliyopita mama yake Bobbi,alikutwa pia kwenye bafu lake amepoteza fahamu baada ya kupitiliza kiwango cha dawa za kulevya na pombe mwishowe kufariki dunia.
Bobbi alikuwa mtoto pekee wa Whitney Houston na Bobby Brown,magwiji wa muziki wa miondoko ya R &B.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni