Wapiganaji
wengi wa Kiislam wa kundi la Islamic State wameripotiwa kuuawa katika
mapigano makali kati ya majeshi ya usalama ya Misri na kikundi hicho
katika peninsula ya Sinai, kaskazini mwa Misri. Mapigano yalidumu kwa
saa kadhaa kuzunguka mji wa Sheikh Zuwaid, kwa serikali kupeleka ndege na
helikopta za kivita.
Mbali na kuuawa kwa wapiganaji wa Islamic State, wanajeshi na raia ni miongoni mwa waliopoteza maisha.Habari kutoka mjini Cairo, Majeshi maalum ya usalama ya Misri yalizingira jengo moja na kuwaua wafuasi tisa wa kikundi cha Muslim Brotherhood. Wizara ya mambo ya ndani imesema watu hao walishukiwa kupanga mfululizo wa mashambulio. Kikundi cha Muslim Brotherhood kimesema wafuasi wake tisa waliuawa kikatili na kimewataka wafuasi wake kufanya maasi dhidi ya Rais Abdel-Fattah el-Sisi.
Wapiganaji wa Islamic State wamekuwa pia wakiendesha mashambulizi katika nchi za Syria na Iraq kwa lengo la kuzitawala nchi hizo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni