Brenda Myers-Powell alikuwa mtoto wakati alipoanza kufanya ukahaba
katika miaka ya sabini. Alizaliwa eneo la Chicago, Marekani na mamake
mzazi alifariki dunia akiwa na miezi sita pakee.
Hapo ilimlazimu
kusalia na bibi yake. Aligundua baadaye kwamba mamake alikufa kutokana
na ulevi wa kupindukia.Kwa sababu bibi yake alikuwa mfanyakazi wa ndani
ilimlazimu Brenda kujipeleka shule na kurejea nyumbani mwenyewe licha ya
kwamba alikuwa kwenye chekechea.Baadhi ya watu walimdhulumu kingono mtoto huyo wakati alipokuwa akitoka chekechea.
Mwanamama huyu alifanya ukahaba kwa miaka 15, wakati huu wote hakuwahi kujiingiza katika mihadarati. Lakini kutokana na mazingira magumu kwenye madanguro ya ukahaba, hakuwa na budi kuanza kutumia mihadarati ili kusahau maisha aliyokua akiishi.
Baada ya ya miaka 25 kama kahaba, siku moja alikutana na mteja ambaye alikuwa katili. Alimtupa nje ya gari lake huku likienda kwa mwendo wa kasi. Brenda alipata majeraha mabaya kiasi cha kupelekwa hospitalini akiwa mahututi.
Lakini madaktari waliokuwa wakimhudumia walimdhihaki kwamba alipata alichotaka na kumsuta kwamba alikuwa amehadaa mteja ndipo akapata adhabu hiyo. Hapo wakawaita polisi kumkamata.
Lakini kwa bahati nzuri daktari mmoja alizungumza na Brenda na kumshauri afike katika kituo cha huduma ya jamii maarufu kama Genesis House. Msimamizi wa kituo hiki alikua Bi Edwina Gateley raia wa Uingereza.
Ni katika kituo cha Genesis Brenda alipata maisha mapya na kuanza safari ya kupona machungu, adhabu na kero za ukahaba. Hakupata shinikizo za kuondoka hadi pale alipohakikisha maisha yake yalikuwa shwari.
Kwa sasa Brenda anawasaidia wanawake na wasichana wanaokimbia ukahaba. Aidha alijaaliwa kuwa na familia, mume na wanawe wawili wa kike. Ana pia wajukuu. Maisha yake ni kuwafundisha soka watoto na kuhakikisha wanaishi kwa maadili mema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni