Mbunge wa
Viti Maalumu kupitia chadema,Rose Kamili,akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo jioni kuhusiana na tuhuma alizozitoa
mume wake kwamba waliishi kwa maisha ya kula mihogo na familia yake ili
kuhakikisha Chadema inastawi na kuimarika jambo ambalo si la kweli
walikuwa na maisha mazuri ya kawaida tu na kusema kuwa Dk.Slaa anapaswa
awaombe radhi wataznzania kwa kufafanisha kula mihogo kuwa ni umaskini
na kuongeza kwa kusema mbona ukienda katika mahoteli makubwa mihogo na
viazi ipo na watu wenye pesa zao wanakula kama kawada.
akizungumzuia
kuhusu matamshi aliyasema Dk.Slaa kwamba haongei na waziri mkuu
mstaafu,Sumaye,mama rose kamili alisema kuwa wiki tatu zilizopita waziri
mkuu huyo mstaafu aliomba namba za dk.slaa akampatia wakaongea vizuri
bila shida yoyote ila anamshangaa juzi aliposema mbele ya waandishi wa
habari kwamba hazungumzi na sumaye.
akizungumzia
kuhusu kuja kwa Lowassa Chadema mama huyo alisema kuwa Dk.slaa
alikuwepo katika kumkaribisha waziri mkuu mstaafu, Edward Lowassa
kujiunga na chama hicho ni jambo la kushangaza akizungumza kwamba
hakushiriki na pia wakati chokochoko hizo za kustaafu ukatibu wake
alisema kuwa viongozi waandamizi wa chama cha mapinduzi walimfuata na
kumshawishi kutoludi kwenye ukatibu mkuu wake huo atapewa ubunge wa
kuteuliwa na rais atakayeapishwa na kupewa uwaziri katika serikali ya
awamu ya tano.
Kamili
alimaliza kwa kutoa rai kwa watanzania wote nchini kutomsikiliza
Dk.Wilbrod Slaa na kuwasihi kuendelea kuwa na matumaini na mgombea wa
urais wa Chadema,Edward Lowassa aliyesimamishwa na chama chao pamoja na
umoja wa katiba ya wananchi (Ukawa) ili kukiondoa madarakani chama
tawala.
Linus Slaa.
Emiliana Slaa.
Mama Rose Kamili akizungumza kwa hisia kali.kushoto ni mtoto wake aliyezaa na Dk.Slaa aitwaye,Emiliana Slaa.
Mama Rose Kamili akizungumza kwa hisia kali.kulia ni mtoto wake, Linus Slaa.
waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini leo
Mbunge wa
Viti Maalumu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Rose Kamili,
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya mume
wake Dk.Wilbrod Slaa kuzungumza wakati akiwa Katibu mkuu wa chadema
familia yake ilikula kwa shida kwa sababu ya kujenga chama hicho jambo
ambalo si la kweli. Wengineo ni watoto wake, Linus Slaa (kulia) na
Emiliana Slaa.
SOURCE:HABARI TANZANIA