Rais wa
Chama cha Wasafirishaji Tanzania (TAT), Zacharia Hans Pope (kushoto),
akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu changamoto
ya sheria ya ongezeko la thamani VAT katika mizigo inayosafirishwa
kwenda nje ya nchi. Kulia ni Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha
Tanzania (TAFFA), Stephen Ngatunga
Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA), Stephen Ngatunga (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa TAT, Omar Kiponza.
Makamu Mwenyekiti wa TAT, Omar Kiponza (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Rais wa Chama cha Wasafirishaji Tanzania (TAT), Zacharia Hans Pope (wa pili kushoto), akiwa na viongozi wengine meza kuu.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
WADAU wa
usafirishaji wa mizigo kwenda nje ya nchi wameiomba serikali kusimamisha
kwa muda sheria ya tozo la VAT katika mizigo inayosafirishwa ili
kulinusuru taifa kiuchumi.
Ombi hilo
limetolewa na Rais wa Chama cha Wasafirishaji Tanzania (TAT), Zacharia
Hans Pope wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo
asubuhi kuzungumzia changamoto ya sheria hiyo.
"Sheria
hii haina manufaa yoyote katika kuinua uchumi wa nchi yetu kwani
imesabisha mizigo kupungua katika bandari yetu kutokana na wadau wa
usafirishaji kuanza kutumia bandari za nchi jirani kwa kuogopa kulipa
kodi hiyo ya mizigo" alisema Hans Pope.
Alisema
hivi sasa katika bandari ya Dar es Salaam kumekuwa na upungufu mkubwa wa
mizigo jambo lililosababisha magari ya mizigo kushindwa kusafiri hivyo
kutishia ajira na maisha ya watu wanaotegemea kuishi kwa kutegemea
usafirishaji.
Makamu
Mwenyekiti wa TAT, Omar Kiponza alisema tozo hiyo ya mizigo
inayosafirishwa nje ya nchi imeleta changamoto kubwa kwa wadau wa
usafirishaji kwani kuna magari zaidi ya 450 ya moja ya kampuni
yaliyokuwa yakienda nchi ya nchi na mizigo wa mwezi yamefungiwa ndani
bila kufanya safari zozote.
Rais wa
Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFFA), Stephen Ngatunga alisema ni
muhimu kwa serikali kuangalia sheria hiyo ili iwe na manufaa kwa nchi
badala ya kuwakandamiza wadau wa usafirishaji.
Alisema
hivi sasa miziogo mingi imekuwa ikipishwa katika bandari za nchi jirani
kwa kukwepa tozo hilo jambo ambali linaweza kuporomosha uchumi wa nchi
unaotegemea sekta ya usafirishaji.
Alisema
hivi sasa usafirishaji wa mizigo katika bandari ya Dar es Salaam umeanza
kudorora kwa kiasi kikubwa na kuiomba serikali kuliangalia jambo hilo
kwa makini ikiwa ni pamoja na kukutana na wadau wa usafirishaji ili
kunusuru jambo hilo.
"Unajua
kupitishwa kwa sheria hiyo kulifanyika haraka bila ya serikali kukutana
na wadau wa usafirishaji ili kujua changamoto zao tunaomba tukutane na
serikali ili kujadili jambo hili kwa kina kabla mambo hayajaharibika
zaidi" alisema Ngatunga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni