Ijumaa, 23 Juni 2017

Idadi ya watu duniani kufika bilioni 10 mwaka 2050

Ripoti ya Umoja wa Mataifa inakadiria idadi ya watu India itaipiku ya China katika kipindi cha miaka saba ijayo na Nigeria inatarajiwa kuipiku Marekani na kuwa taifa la tatu duniani lenye idadi kubwa ya watu ifikapo 2050
Ripoti hiyo iliyotolewa na idara ya uchumi na masuala ya kijamii ya shirika la  kushughulikia idadi ya watu duniani katika Umoja wa Mataifa inakadiria kuwa idadi ya hivi sasa ya watu duniani ya takriban bilioni 7.6 itaongezeka hadi watu bilioni 8.6 ifikapo mwaka 2030, bilioni 9.8 ifikapo 2050 na bilioni 11.2 ifikapo mwaka 2100.
Inaripotiwa kuwa karibu watu miliioni 83 wanazaliwa duniani kila mwaka, dalili zinaoonyesha ongezeko litakaloendelea hata kama viwango vya uzazi vitashuka kama inavyoshuhudiwa tangu miaka ya 1960.

Jumatano, 21 Juni 2017

Shambulio la bomu Brussels: mtuhumiwa auawa

Polisi katika eneo la tukio

Polisi katika eneo la tukio
Wanajeshi wa Ubelgiji wamemuua kwa kumpiga risasi mlipuaji wa bomu wa kujitoa muhanga, katika kituo kikuu cha reli mjini Brussels.
Idara ya polisi imesema kuwa mtu huyo alikuwa amevalia kile kilichoonekana kuwa mkanda wa vilipuzi na kuwa kulitokea mlipuko mdogo.
Waendesha mashtaka wanasema kuwa mshukiwa huyo amefariki.
Watu waliokuwa katika kituo Kikuu cha mabasi mjini Brussels na eneo la karibu la mnara ambalo hufurika watalii wote waliondolewa.
Wanajeshi wamekuwa wakilinda doria mjini Brussels tangu kulipotokea shambulio la kujitoa mhanga katika eneo la Uwanja wa ndege na kwenye mfumo wa usafiri wa chini ya ardhi mwaka uliopita .

Jumanne, 20 Juni 2017

Je uko tayari kuambukizwa ugonjwa kwa malipo ya pauni 3,526?

Watafiti katika chuo kikuu cha Southampton University wanawapatia watu pauni 3,526 ili kukubali changamoto hiyo.

Watafiti katika chuo kikuu cha Southampton University wanawapatia watu pauni 3,526 ili kukubali changamoto hiyo.
Je ni pesa ngapi zinaweza kukushawishi kukubali kuambukizwa kikohozi ili kusaidia uvumbuzi wa kisayansi.
Watafiti katika chuo kikuu cha Southampton University wanawapatia watu pauni 3,526 ili kukubali changamoto hiyo.
Wanataka kutengeneza chanjo bora ili kuwalinda watoto, na watu wazima ambao wapo hatarini kuambukizwa ugonjwa huo.
Ili kusaidia ni sharti uwe na umri wa kati ya miaka 18-45, uwe na afya bora, uwe tayari kutengwa kwa siku 17 na kuimba.
Kikohozi ni ugonjwa unaoweza kuambukizwa kwa haraka na huenezwa kupitia hewa ya kikohozi kutoka kwa mtu ambaye ameambukizwa .
Kundi hilo kutoka mjini Southampton linataka kuwaambukiza watu walio na afya nzuri kwa kuwawekea puani viini vinavyosababisha maambukizi hayo na kuwachunguza.
Baadhi ya watu waliojitolea watakuwa wagonjwa, lakini wanasayansi wanataka wale ambao hawatakuwa na dalili zozote licha ya kuwekewa viini hivyo katika pua zao.
Kile wanachotafuta ni wale wanaobeba viini hivyo kwa siri na watu ambao wanakinga ya ugonjwa huo.
Wale wanaobeba ugonjwa huo kwa siri huwaambukiza watu wengine lakini huwa hawapatwi na ugonjwa huo.
Huonekana kuwa na kinga ya kutosha ya kukabiliana na ugonjwa huo licha ya kwamba hawajapewa chanjo.

AFUNGISHWA NDOA NA MAREHEMU NCHINI MSUMBIJI

Dola za Marekani

Mtu mmoja kusini mwa Msumbiji katika mkoa wa Inhambane alilazimika kumlipia mahari mkewe aliyefariki wikendi iliopita kulingana na chombo cha habari cha taifa.
Baada ya mkewe kufariki kutokana na matatizo ya kujifungua, nduguze walimlazimisha mpenziwe kulipa ''Lobolo'', wakionya kwamba la sivyo hatozikwa.
Nduguze walimshutumu kijana huyo kwa kushindwa kuafikia majukumu yake ikiwemo kutambulishwa kwa jamaa na ndugu za mwanamke huyo kabla ya janga hilo kutokea.
Ili kuhakikisha kuwa mazishi hayo yanafanyika, kijana huyo alilazimika kumnunulia nguo na viatu marehemu mkewe, kukubali kulipa zaidi ya dola 800 (sawa na shilingi za Kitanzania1,760,000) na kufanya haruasi mnamo tarehe 15 mwezi Disemba.
Nduguye kijana huyo Irmao do Jovem alielezea matatizo yao.
''Tulijaribu kuchangisha fedha walizotaka, lakini tuliweza kuchangisha dola 178 (sawa na shilingi za Kitanzania 387,200) tu. Hivyobasi ilibidi kuweka ahadi ya kulipa fedha zilizosalia siku ya harusi''.
Huku ikiwa familia ya kijana huyo imekubali kulipa, walishutumu tabia ya familia ya mwanamke huyo.
Hatahivyo, ni utamaduni miongoni mwa makabila mengi nchini Msumbiji hususan iwapo mwanamume anaamua kuishi na mwanamke bila kufuatilia utamaduni wa kumuoa mwanamke huyo.
Hili ni funzo kwa vijana wengi ambao wanapenda kuishi na wanawake bila kujitambulisha kwa wazazi wa mwanamke husika na kufunga nao ndoa.