Ijumaa, 20 Oktoba 2017

Kifungo cha waliokamatwa wakibusiana chaendelezwa na mahakama ya rufaa nchini Tunisia

Kifungo cha waliokamatwa wakibusu chadumishwa na mahakama Tunisia

Kifungo cha waliokamatwa wakibusu chaendelezwa na mahakama Tunisia

Mahakama ya rufaa nchini Tunisia imeamuru kuendelezwa kwa hukumu ya wapenzi wawili waliokamatwa mwezi Septemba kwa kubusu wakiwa ndani ya gari lao.
Nessim Ouadi, ambaye ni raia wa Ufaransa pia alilaumiwa kwa kupuuza maagizo ya baada ya kukamatwa pamoja na mpenzi mwanamke raia wa Tunisia.
Wawili hao walipewa vifungo vidogo ikiwa ni miezi minne kwa mwanamume na miwili kwa mwanamke tofauti na walivyopewa mwezi Oktoba.

Kesi hiyo ilisababisha malalamiko katika mitandao ya kijamii na kuzua mjadala nchini Tunisia kuhusu maadili katika maeneo ya umma na wajibu wa polisi.
Mkuu wa mshataka alisema kuwa kesi hiyo imeripotiwa kwa njia isiyofaa na vyombo vya habari vya kimataifa na kuwa wawili walikuwa uchi na walikuwa wakifanya mapenzi wakati walisimamishwa na polisi. Jambo hili linazua mawsali mengi kwa sababu sio rahisi watu kuendesha gari huku wakifanya mapenzi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni