Jumatano, 9 Novemba 2016

Donald Trump ashinda uchaguzi wa Rais wa Marekani

Wamarekani wamchagua Trump kuwa rais wao
Wamarekani wamemchagua Donald Trump kuwa rais wa 45 wa nchi hiyo. Amejipatia sauti 276 dhidi ya 218 za wawakilishi wa majimbo. Rais mteule Trump amewahutubia wafuasi wa chama chake na wamarekani kwa jumla. Mgombea wa chama cha Democrats Hillary Clinton amekubali kushindwa na ameshazungumza kwa simu na Donald Trump kumpongeza.

MTOTO ASIPEWE JINA LA BABA PEKEE: ITALIA

Mwanamke mjamzito

Hadi sasa akina mama wa Italia wamekuwa wakikataliwa kuwapatia watoto wao majina ya baba zao
Mahakama ya katiba ya Italia imetoa hukumu dhidi ya sheria inayompatia moja kwa moja mtoto anayezaliwa ndani ya ndoa jina la baba yake.
Mawakili walidai kuwa kuzuwia familia kuwapatia watoto wao majina ya babu zao wazaa mama ni ubaguzi dhidi ya wanawake.

Jumanne, 8 Novemba 2016

WEZI WA KENYA KIBOKO: WAIBA MASHINE YA ATM NAIROBI

 Benki ya Equity
Picha ya Benki ya Equity, Kenya

Polisi nchini Kenya katika jiji kuu Nairobi wamemkamata mlinzi wa Benki ya Equity kuhusiana na wizi mwishoni mwa wiki ambapo wezi walitoweka na mtambo wa kutoa pesa, ATM.

Wezi hao walitoweka na kiasi cha pesa ambacho hakijajulikana kwa sasa wakati wa wizi huo Jumamosi.
Wezi hao walichimba ukuta wa nyuma wa Benki hiyo na kutoweka na sanduku la uhifadhi wa pesa pamoja na mtambo wa ATM, pesa zikiwa ndani.
Washukiwa waliweza kuzima kamera za CCTV na pia kengele ya usalama kabla ya kutekeleza wizi huo.

Akizungumza na BBC, kamanda wa jimbo la Nairobi Japheth Koome amesema kwamba polisi waliweza kupata mitungi ya gesi na vifaa vingine ambavyo hutumuka kukata chuma.

Alipoulizwa kama wezi siku hizi wamepata maarifa utadhani wanaiga filamu, alisema kwamba kwa siku za hivi karibuni wizi wa benki unazidi kubadilika sana.

Mwaka uliopita, wezi waliojifanya wakaguzi wa hesabu katika benki hiyo walitoweka na dola za Marekani 300,000

SAMWEL SITTA HATUNAYE

4494_b.jpg
Tunasikitika kuwataarifu kuwa mzee wetu mpendwa Samwel Sitta amefariki dunia katika Hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani saa 7:30 kwa muda wa Ujerumani alikokuwa akitibiwa ugonjwa wa Saratani ya Tezi Dume.

Historia yake:

  ​
Samuel John Sitta alizaliwa Desemba 18, 1942 huko wilayani Urambo Mkoa wa Tabora. Sitta alisoma Shule ya Msingi Urambo kati ya mwaka 1950 – 1953, kisha alikwenda Wilaya ya Sikonge mwaka 1954 - 1957 na kuendelea na masomo ya “Middle School” katika shule ya “Sikonge Middle School”. Baadaye mwaka 1958 – 1963 alianza masomo ya sekondari Shule ya Wavulana Tabora yaani “Tabora Boys” kidato cha I – IV na cha V – VI.

Mara tu baada ya kuhitimu masomo ya sekondari, Sitta alijiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kusomea Shahada ya Sheria (L LB) mwaka 1964 na kuhitimu mwaka 1971.

Ijumaa, 28 Oktoba 2016

MPIGA MBIZI AIBUA BOMU LA NYUKLIA

 Bomu la nyuklia lililopotea
Bomu la nyuklia lililopotea

Mpiga mbizi mmoja huenda amegundua bomu la kinyuklia la Marekani ambalo lilipotea katika pwani ya Canada.

Sean Smyrichinsk alikuwa akiogelea akiwatafuta majongoo wa baharini karibu na Colombia inayomilikiwa na Uingereza wakati alipogundua chuma kikubwa kilichofanana na kisahani .

Idara ya ulinzi nchini Canada inaamini huenda ni bomu la kinyuklia kutoka kwa ndege ya kivita aina ya US B-36 Bomber ilioanguka katika eneo hilo 1950.

Serikali hiyo haiamini kwamba bomu hilo lina Nyuklia.
Canada tayari imetuma ndege ya wanamaji katika eneo hilo karibu na Haida Gwaii ili kulikagua bomu hilo.

TB Joshua: Bi Clinton atashinda urais Marekani

Muhubiri TB Joshua

Muhubiri TB Joshua amesema kuwa Bi Clinton atashinda kwa ushindi mdogo dhidi ya mpinzani wake
 
Muhubiri maarufu wa vipindi vya Televisheni nchini Nigeria TB Joshua amesema ametabiri " kwamba Hillary Clinton atamshinda Donald Trump" katika uchaguzi wa urais wenye ushindani mkali tarehe 8 Novemba mwaka huu.

Katika ujumbe alioutuma kwenye ukurasa wake wa Facebook TB Joshua amesema kuwa Bi Clinton atashinda kwa ushindi mdogo, lakini atakabiliwa na changamoto nyingi - likiwemo jaribio la kupiga kwa kura ya kutokuwa na imani dhidi yake.

TB Joshua ni mmoja wa viongozi wa kidini wenye ushawishi na utata barani Afrika, huku wengi wa wafuasi wake wakiamini kuwa "utabiri " wake ni wa uhakika.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA BALOZI WA HESHIMA WA TANZANIA NCHINI FINLAND




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Mhe. Vesa Viitaniem (kushoto), Ikulu jijini Dar es Salaam, katikati ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Mama Anna Mkapa .

Alhamisi, 27 Oktoba 2016

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WANNE KUTOKA NCHI MBALIMBALI, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimkaribisha ofisini kwake Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad (kushoto) kwa ajili ya kufanya mazungumzo naye kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Norway na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri huyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya. Picha na zote Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

BREAKING NEWS DARASA LA SABA MATOKEO HAYA HAPA

BREAKING NEWSS:HAYA NDIO MATOKEO YA DARASA LA SABA

Kuyatazama matokeo ya darasa la saba mwaka 2016;

WAZIRI MAKAMBA AKAMILISHA ZIARA KATIKA MKOA WA KATAVI

 Bibi Josephine Rupia, Mkuu wa Idara ya Maliasili Halmashauri ya Mpanda akitoa maelezo ya Mto Katuma kupoteza mwelekeo wa kutiririsha maji katika mkondo wake kama ilivyokuwa hapo awali.
Wengine katika picha ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga