Nyoka huyo anaaminika kutoweka baada ya kisa hicho.
Mwanamume mmoja
katika jimbo la Florida nchini Marekani ambaye alijaribu kumbusu nyoka
na badala yake nyoka huyo akamuuma, anaendelea kupata matibabu
hospitalini.
Nyoka huyo aliokotwa na Charles Goff, mkazi wa kaunti ya Putnam kaskazini mwa jimbo la Florida siku ya Jumatatu.
Siku moja baadaye jirani yake ambaye alitajwa na kituo cha CBS kama Ron Reinold alianza kucheza na nyoka huyo kwa kujaribu kumbusu.
Bwana Reinold alisafirishwa kwa njia ya ndege na kwa sasa anaendelea kupata nafuu hospitalini,.
Kijana mmoja alisema, "nitambusu mdomoni," ndipo nyoka huyo
akamuuma usoni, bwana Goff alililiambia shirika la habari la Action
News Jax.
Kituo cha First Coast News kilisema kuwa muathirika
alikuwa na fahamu lakini katika hali yake ilikuwa mbaya. Nyoka huyo anaaminika
kutoweka baada ya kisa hicho.
Haijulikani sababu iliyochangia bwana Reinold ajaribu kumbusu nyoka huyo.
JW Leford amekuwa akitumia dawa ya kupunguza maumivu
ya nevi ambazo mawakili wake wanasema huenda zikabadili utendakazi wa
ubongo wake.
Mfungwa mmoja
anayesubiri kunyongwa katika jela moja katika jimbo la Georgia nchini
Marekani amewasilisha ombi la kuuawa kwa kuumiminiwa risasi kwa sababu
kifo cha kuuawa kwa kudungwa sindano kina uchungu mno.
JW Leford
amekuwa akitumia dawa ya kupunguza maumivu ya neva ambazo mawakili wake
wanasema huenda zikabadili utendakazi wa ubongo wake na kumfanya kuwa
na uchungu mkali kinyume na katiba.
Ledford alihukumiwa 1992 kwa kumuua jirani yake.
May Chen Anasema kwamba ameamua kuafikia ndoto
yake kupitia kupiga picha za harusi. Alijichagulia marinda yote manne na
vito alivyovaa
Mwanamke mmoja ambaye anaugua saratani ya matiti amejioa mwenyewe baada ya kusubiri mchumba kwa muda mrefu.
May
Chen mwenye umri wa miaka 28 kutoka Taiwan ameambia BBC kwamba anaugua
ugonjwa huo lakini hajakubali sababu hiyo kuhujumu ndoto yake ya
kuolewa.
''Nimekuwa nikisubiri mtu kujitokeza na kusema kwamba
angependa kufunga ndoa nami mbali na kupiga picha za harusi nami
aliambia BBC .
Anasema kwamba wakati unapohisi kwamba huna miaka mingi ya kuishi huna budi kujifanyia maswala ambayo yamekuwa ndoto yako.
Anasema kwamba ameamua kuafikia ndoto yake kupitia kupiga picha za harusi. Alijichagulia marinda yote manne na vito alivyovaa.
Chumba cha kuchomea
maiti katika jimbo la Ohio nchini Marekani kiliungua wakati
kilipokuwa kikitumika kuchoma mwili wa mfu aliyenenepa kupita kiasi
kulingana na mmiliki wa chumba hicho.
Don Catchen alisema kuwa maiti hiyo ilisababisha moto uliochoma chumba hicho katika mji wa Cincinati.
Mafuta
yaliokuwa katika mwili huo yalichomeka katika viwango vya juu vya joto
na kusababisha moto huo kulingana na afisa mkuu wa zima moto.
Hata hivyo hakuna eneo jingine la chumba hicho lililochomeka kulingana na Catchen.
Picha ya binti
mfalme Charlotte imetolewa na Kensington Palace kuadhimisha siku yake ya
kuzaliwa anapotimia umri wa miaka miwili siku ya Jumanne.
Picha hiyo aliyochukuliwa na mama yake, inamuonyesha Charlotte nyumbani mwa familia.
Familia ilitoa picha ya Charlotte sawa na hiyo mwaka uliopita alipotimia umri wa mwaka mmoja.
Kensington Palace ilisema kuwa kila mmoja anafurahia picha hiyo vile wao wenyewe wanavyoifurahia. Alipigwa picha mara ya kwanza akitolewa St Mary's Hospital, na wazazi wake
Familia inatarajiwa kumuandalia karamu binti mfalme huyo.
Familia
huzuia binti mfalme huyo kuonekana kwa umma lakini alipigwa picha
wakati wa ibada ya krismasi katika kijiji cha Bucklebury.
Pia
alionekana wakati familia ilifanya ziara nchini Canada ambapo alionekana
mara kadha ikiwemo waki wa karamu ya watoto huko Victoria Prince George na Princes Charlotte
Princess Charlotte
Princess Charlotte
Familia huzuia binti mfalme huyo kuonekana kwa umma
Kerengende wa kike hujifanya wamekufa ili kukwepa tendo la ngono na wenzao wa kiume
Utafiti mpya umebaini kwamba kerengende wa kike huwa anajifanya kuwa amekufa ili kukwepa wenzao wa kiume.
Rassim
Khelifa, kutoka chuo kikuu cha Zurich Switzerland, anasema kwamba
aliona kerengende wa kike aliyekuwa akifuatwa na wa kiume ili kufanya
mapenzi, akijiangusha na kulala kana kwamba amefariki, hadi pale
kerengende wa kiume alipoondoka. Ripoti hiyo imechapishwa kwenye jarida la ikolojia. Bwana
Khelifa amesema kuwa kerengende wa kike hunyanyaswa kwa sababu huwa
hawana ulinzi baada ya kutaga mayai ikilinganishwa na kerengende
wengine.
Athaya Slaetalid na mumewe Jan pamoja na mwana wao Jacob
Kuna upungufu wa wanawake katika kisiwa cha Faroe.
Hivyo basi wanaume katika kisiwa hicho wanatafuta wanawake kutoka maeneo mengine kama vile mataifa ya Thailand na Ufilipino.
Lakini je ni changamoto gani zinazowakumba wanawake wanaoelekea katika kisiwa hicho.
Wakati
Athaya Slaetalid alipoelekea katika kisiwa hicho ambapo kipindi cha
majira ya baradi huchukua muda wa miezi sita alikuwa akikaa karibu na
kikanza ama heater kwa jina la Kiingereza kwa siku nzima.
''Watu walikuwa wakiniambia niende nje kwa sababu kuna jua lakini nilisema'': ''Hapana niacheni, nahisi baridi sana''.
Kuhamia katika kisiwa hicho miezi sita iliopita ilikuwa vigumu kwa Bi Athaya aliyekiri.
Alikutana
na mumewe Jan alipokuwa akifanya kazi na rafikiye mmoja wa kisiwa hicho
ambaye alikuwa ameanza biashara nchini Thailand.
Jan alijua mapema kwamba kumpeleka mkewe katika utamaduni huo, hali ya hewa itakuwa changamoto kubwa. Kisiwa cha Faroe chenye upungufu wa wanawake
"Nilikuwa na wasiwasi kwa sababu kila kitu
alichokiacha nchini Thailand kilikuwa tofauti na kile alichokuja kuona
katika kisiwa cha Faroe'', alisema.
''Lakini kwa sababu namjua Athaya nilijua ataingiliana na hali ya hewa''.
Kufikia sasa kuna takriban wanawake 300 kutoka Thailand na Ufilipino wanaoishi katika kisiwa cha Faroe.
Haionekani
kuwa idadi kubwa lakini kisiwa hicho chenye idadi ya watu 50,000 sasa
wanawakilisha watu walio wachache katika visiwa hivyo 18 kati ya Norway
na Iceland.
Katika miaka ya hivi karibuni visiwa vya Faroe
vimepata upungufu wa idadi ya watu huku vijana wakiondoka ili
kutafuta elimu na huwa hawarudi.
Wanawake wameamua kuishi ughaibuni.
Viongozi watano wa muungano wa upinzani Kenya (NASA)
Muungano wa vyama
vya upinzani nchini Kenya unatarajiwa kumtaja atakayewania urais dhidi
ya Rais Uhuru Kenyatta kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti.
Tangazo
hilo litafanyika huku nchi hiyo ikimaliza shughuli kura za mchujo za
vyama, ambazo zimekumbwa na vurugu na madai ya kuiba kura.
Maelfu ya wafuasi wa upinzani wamefika katika uwanja wa Uhuru Park kuhudhuria mkutano huo.
Huku
zikiwa zimesalia siku 102 tu kabla ya uchaguzi, muungano mkuu wa
upinzani Kenya ulikuwa na muda mdogo kumtaja kiongozi wao. Muungano huo
wa National Super Alliance, yaani NASA, una wanaume watano wote
wanaotaka kuongoza, lakini inatarajiwa kuwa jopo litamchagua Raila
Odinga.
Vigogo wengine kwenye muungano huo ni makamu wa rais wa
zamani Kalonzo Musyoka, makamu wa rais wa zamani Musalia Mudavadi,
waziri wa zamani wa mambo ya nje Moses Wetangula na mwenyekiti wa zamani
wa baraza la magavana Isaac Ruto.
Bw Ruto, anayeongoza chama cha
Chama cha Mashinani (CCM) alikuwa kwenye muungano wa vyama vinavyomuunga
mkono Bw Kenyatta kabla ya kuhama na kuunda chama chake.
Bw Odinga ndiye kiongozi wa chama cha ODM, ambacho kina wabunge wengi zaidi katika Bunge la sasa.
Iwapo atachaguliwa kuwa mwaniaji wa NASA, basi itakuwa ni mara ya nne kwake yeye kupigania urais.
Kiongozi
huyo bado anasisitiza kuwa alishinda uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo rais
wakati huo, Mwai Kibaki alitangazwa mshindi, na kuzua tafrani nchini
Kenya ambapo watu zaidi ya elfu moja waliuawa.
Huku hayo yakijiri, wanasiasa wengi wanaendelea kupoteza viti vyao kwenye kura za mchujo. Wafuasi wa chama cha Wiper chake Bw Kalonzo Musyoka
Wafuasi wa chama cha ODM uwanjani Uhuru Park
Bw Musyoka, Bw Odinga na Bw Wetangula
Wakenya kwenye mtandano wamekuwa wakiendesha kampeni
inayoitwa Opresheni Fagia Wote, na mwandishi wetu Ferdinand Omondi
anaripoti anasema huenda wanafanikiwa.Baadhi ya maeneo ya uchaguzi yamemfuta kazi Gavana, Seneta, wabunge na madiwani wote.
Kampeni
ya Fagia Wote inapania kuonyesha ghadhabu ya Wakenya kwa jinsi taifa
hilo limeendeshwa kwa miaka minne iliyopita. Kumezuka vurugu kwenye
sehemu kadhaa nchini na pia madai ya kuiba na kununua kura.
Askofu
mmoja wa kike, Margaret Wanjiru ambaye amewahi kuwa waziri, ambaye kwa
sasa alikuwa anawania kuwa Gavana mpya wa Nairobi, alilala kwenye seli
ya Polisi alipokamatwa jana kwa madai ya kuzua rabsha katika kituo cha
uchaguzi.
Kura za mchujo zinafaa kumalizika Jumapili.
Uchaguzi mkuu utafanyika tarehe 8 Agosti.
Mshike mshike wa
kuwania ubingwa wa ligi kuu England umeendelea kushika kasi ambapo
Tottenham Hotspur walipata ushindi ugenini wa bao 1-0 dhidi ya Crystal
Palace.
Bao pekee la Spurs katika mchezo huo lilifungwa na kiungo
Christian Eriksen, katika dakika ya 78 ya mchezo na hivyo kuendelea
kuwakimbiza vinara wa ligi hiyo Chelsea, wanaongoza ligi kwa alama 78
huku Spurs wakiwa nafasi ya pili kwa alama 74. Beki wa Arsenal Nacho Monreal akishangalia
Nao washika mititu wa London Arsenal, walipata
ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Leicester City, bao la kujifunga la beki wa
Leicester Robert Huth, ndio liliwapa vijana wa Wenger alama tatu muhimu
na kusogea mpaka nafasi ya sita katika msimamo wa ligi.
Vibonde wa
ligi Middlesbrough wakautumia vyema uwanja wa nyumbani wa Riverside
kuwa kuwachapa kwa bao 1-0 vibonde wengine wa ligi Sunderland ambao
ndio wanaburuza mkia katika ligi hiyo
Miamba ya soka la
Hispania vilabu vya Barcelona na Real Madrid vimendelea kutamba katika
ligi hiyo kwa kupata ushindi wa mabao mengi katika michezo yao.
Barcelona
waliichapa timu inayoburuza mkia katika ligi Osasuna, kwa mabao 7 -1
mabao ya Barca yakifungwa na Lionel Messi aliyefunga mabao mawili, Andre
Gomes, nae akafunga mawili kinda Francisco Alcacer, akatupia nae
magoli mawili huku Javier Mascherano, akifunga bao moja. wachezaji wa Real Madrid wakipongezana
Real Madrid wakiwa ugenini katika dimba la Municipal
de Riazor, waliwafunga Deportivo La Coruna, kwa mabao 6-2, mabao ya
Real yalifungwa na James Rodriguez, aliyefunga mara mbili na mengine
yakifungwa na Alvaro Morata, Lucas Vazquez, Isco na kiungo Casemiro
Leganes wakashinda kwa 3 - 0 dhidi ya Las Palmas, Nao Valencia wakalala nyumbani kwa kufungwa 3-2 na Real Sociedad.