Wezi katika mji wa
Mumbai magharibi mwa India walitekeleza wizi kwenye benki moja
inayomilikiwa na serikali baada ya kuchimba njia ya chini kwa chini ya
urefu wa futi 25 (mita 8).
Walichimba njia hiyo kwa miezi kadha.
Polisi wameambia BBC kwamba pesa taslimu pamoja na vito vya thamani isiyojulikana viliibiwa.
Maafisa wanaamini kwamba wezi hao walikodisha chumba karibu na Benki ya Baroda kuwawezesha kuchimba njia hiyo.
Wanadaiwa kuendesha biashara ya kuuza mboga na matunda katika kiduka chao kuficha mipango yao.
Wezi hao walitoweka tangu Jumamosi usiku baada ya kutokea kwa wizi huo. Polisi wanaamini wezi hao walikodisha duka karibu na benki hiyo
Haijabainika ni vipi wanaume hao walifanikiwa kuchimba njia hiyo kwa miezi kadha bila kugunduliwa.
Vyombo vya habari nchini India vimezungumza na wateja wa benki hiyo ambao vitu vyao vya thamani viliibiwa.
"Akiba
yangu yote ilikuwa imewekwa kwenye sefu. Vito ambavyo tumemiliki kwa
vizazi kadha, vimeibiwa," Dagdu Gavani, mmoja wa wateja aliambia Mumbai
Mirror.
Wafanyakazi wa benki hiyo iliyo viungani mwa mji wa Mumbai waligundua wizi huo Jumatatu na kuwafahamisha polisi.
Polisi wameambia BBC kwamba sefu 30 kati ya 225 kwenye benki hiyo ziliporwa.
Washukiwa bado hawajatambuliwa. Benki ya Baroda humilikiwa na serikali
Mawaziri
kadhaa katika serikali ya Rais Robert Mugabe wamekamatwa baada ya Jeshi
la Ulinzi kuonyesha uwezo wake na kushikilia majengo yakiwemo ya
shirika la utangazaji (ZBC).
Milipuko
mikubwa ilisikika na ikafuatiwa na ya bunduki katika maeneo
yanayokaliwa na watu maarufu ya Borrowdale usiku kucha hali iliyozidisha
hofu kwamba jeshi lilikuwa kazini.
Shirika
la TimesLIVE limeripoti kwamba waliokamatwa ni watu maarufu kutoka
kundi la G40 ndani ya chama cha Zanu PF lililokuwa likiongozwa na
memsapu wa Rais Mugabe, Grace Mugabe.
Baadhi
ya watu waliokamatwa ni Waziri wa Elimu Jonathan Moyo‚ Serikali za
Mitaa Saviour Kasukuwere na Waziri wa Fedha Ignatius Chombo.
Jeshi
limesema katika taarifa yake iliyosomwa na msemaji wake moja kwa moja
kupitia ZBC kwamba Rais Mugabe yuko “salama na mwenye afya njema”.
Taarifa hii imekuja baada ya askari wakiwa na silaha jana Jumanne kwenda
katikati ya mji wakiwa kwenye magari ya kijeshi.
Shirika la Utangazaji la Zimbabwe ambalo majengo yake yako eneo la Pocket Hills jijini Harare lilitekwa saa 10:00 alfajiri.
Soma: Jeshi lasema Mugabe, familia wako salama
Msemaji
wa jeshi, Meja Jenerali Sibusiso Moyo alitangaza kwamba jeshi lilikuwa
linadhibiti kwa lengo la kuhakikisha linawashughulikia “wahalifu”
wanaomzunguka Mugabe.
“Sisi
tunawalenga wahalifu wanaomzunguka yeye (Mugabe) wanaofanya uhalifu
ambao unawasababishia watu mateso katika Nyanja za kijamii na kiuchumi
hapa nchini na kisha tutawafikisha kwenye vyombo vya sheria‚” alisema
Moyo.
Jengo la Makao makuu ya shirika la kuzalisha na kusambaza umeme, TANESCO
Katika ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa barabara
katika eneo la Ubungo mjini Dar es salaam,Rais Magufuli ameagiza sehemu
ya jengo ambalo ni makao makuu ya shirika linalozalisha na kusambaza
umeme, TANESCO, kuwekwa alama ya 'X' kuashiria jengo hilo libomelewe. Jengo lingine ambalo litaathiriwa na agizo hilo ni jengo la wizara ya maji ambalo lipo jirani. Imeagizwa majengo hayo kubomolewa kutokana na kuwa yamejengwa katika sehemu ya hifadhi ya barabara. Zoezi
la bomoa boma limekuwa likiendelea, ambapo majengo pembezoni ya
barabara inayounganisha mji wa Dar es salaam na maeneo mengine ya nchi
yameathirika. Wakaazi wengi waliokuwa wakiishi katika maeneo yanayodaiwa
kuwa katika hifadhi ya barabara wamepoteza makazi yao. CHANZO: BBC
Ufyatuaji wa risasi kusherehekea swala fulani katika eneo la mashiriki ya kati ni kitu cha kawaida
Bwana harusi moja nchini Misri amejeruhuwa vibaya baada kupigwa na risasi iliokuwa imefyatuliwa ili kusherehekea harusi yake.
Bwana harusi huyo alipata majeraha mabaya katika sehemu yake ya siri , nyongani na mkononi na anatibiwa hospitalini.
Osman
al-Alsaied mwenye umri wa miaka 28 alikuwa akisherehekea usiku wake wa
mwisho akiwa kapera wakati silaha hiyo ilipofyutuliwa upande wake badala
ya hewani.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa bunduki hiyo ilifyatuliwa kiuzembe na mwananume mwenye umri wa miaka 26.
Wanasema kuwa alitoroka muda mfupi baadaye baada ya kisa hicho lakini akakamatwa na sasa anahojiwa.
Ripoti
za kisa hicho zimechochea hisia kali katika mtandao wa kijamii huku
wengi wakitaka sherehe ya kufyatua risasi hewani kusitishwa. Sherehe za harusi nchini Misri hupendwa sana
Iwapo unafyatua risasi wakati unasherehekea furaha yako je itakuwaje wakati unapokasirika, ujumbe mmoja wa Twitter uliuliza.
Kulikuwa na kisa kama hicho katika harusi nchini Misri mwezi uliopita kulingana na mtandao wa Stepfeed.
Katika kisa hicho bwana harusi alifanyiwa upasuaji na matibabu baada ya risasi kumpiga katika nyonga yake
Mahakama ya juu nchini Kenya inasikiliza kesi ya kupinga ushindi wa Uhuru Kenyatta
Kwa mara ya pili
katika chini ya kipindi cha miezi mitatu, macho yote sasa yanaangazia
mahakama ya upeo wa juu zaidi Kenya, itakayoamua iwapo ushindi wa rais
Kenyatta, ni halali au la.
Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi
wa uchaguzi wa urais Kenya na tume ya Uchaguzi IEBC, baada ya uchaguzi
wa marudio ya Oktoba 26.
Kesi tatu zimewasilishwa mbele ya majaji 6
wanaoongozwa na jaji mkuu David Maraga, mbili zikitaka ushindi wa rais
Kenyatta ubatilishwe, huku moja ikitaka viongozi wa upinzani wakiongozwa
na Raila Odinga wachukuliwe hatua kwa madai ya kuchochea wafuasi wao
kususia uchaguzi, na kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi. Rais Uhuru Kenyatta
Kesi za kubatilisha ushindi wa rais Kenyatta
zimewasilishwa kwa misingi kwamba tume ya uchaguzi ilikosa kuagiza
uteuzi mpya wa chama ufanyike baada ya mahakama ya upeo wa juu zaidi
kufutilia mbali ushindi wa rais Kenyatta mwezi Agosti.
Mahakama ina chini ya siku saba kusikiliza na kuamua kesi hizo tatu. Kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Amolo Odinga
Uamuzi rasmi unatarajiwa kutolewa tarehe 21 mwezi huu.
Wafanyakazi wa nyumbani kutoka Tanzania wanadhulumiwa uarabuni
Wafanyakazi wa kike wa nyumbani kutoka nchin
Tanzania walio nchini Oman na milki ya nchi za kiarabu UAE,
wanadhulumiwa kimwili na kingono, wakiwa wanafanya kazi masaa mengi na
wakilipwa mishahara midogo, kwa mujibu wa shirika la kitetea haki za
binadamu, Human Rights Watch (HRW).
Kwenye ripoti iliyotelewa leo, HRW ilisema kuwa kuna maelfu ya wafanyakazi wa nyumbani kutoka Tanzania wako nchini Oman na UAE.
Watafiti
wake waliwahoji 50 kati yao na kugundua kuwa karibu wote walipokonywa
pasipoti zao walipowasili na kulazimiswa kufanya kazi hadi masaa 21 kwa
siku bila kupumzika.
Wafanyakazi waliotoroka waajiri dhalimu na
maajenti walisema kuwa polisi au balozi zao ziliwalazimisha kurudi la
sivyo wangekosa mishahara yao hali iliyowachukua muda mrefu kutafuta
pesa za kuwawezesha kurudi nyumbani.
Walisema kuwa walilipwa pesa
kidogo kuliko zile waliahidiwa, au walikosa kulipwa kabisa,
wakalazimishwa kula chakula kulichooza au mabaki ya chakula na kutukanwa
kila siku, na pia kudhulumiwa kingono.
Mara ya mwisho Italia kushindwa kufuzu kushiriki mashindano haya ilikuwa mwaka 1958
Mabingwa mara nne
wa kombe la dunia Italia, wameshindwa kufuzu fainali za mwa 2018 nchini
Urusi ikiwa ni mara ya kwanza tokea mwaka 1958 baada ya kutoka suluhu ya
bila kufungana na Sweden.
Hii ina maana kwamba Azzurri watayakosa mashindano hayo kwa mara ya pili tokea kuanzishwa, mara ya kwanza ilikua mwaka 1930. Baada ya mchezo huo mlinza mlango wa muda mrefu Gianluigi Buffon ametangaza kustaafu soka la kimataifa
Kiungo Jakob Johansson wa Sweden aliyefunga goli
katika mzunguko wa kwanza alikuwa katika kiwango bora na kuwadhibiti
vyema Italia katika uwanja wa San Siro.
Wengi walitaraji Italia kushinda mchezo huu kwa sababu lukuki ikiwemo historia sambamba na kucheza nyumbani.
Italia walitawala mchezo kwa asilimia 75 na kupiga mashuti 27 lakini bahati haikuwa upande wao. Wachezaji wa Sweden wakisherehekea kufzu.Nusura mshambuliaji Stephan El Shaarawy aandike bao kwa upande wa Italia lakini juhudi za mlinda mlango wa Sweden Robin Olsen zilizima ndoto yake.
Matokeo haya yanaifanya Sweden kushiriki mashindano haya tokea mwaka 2006 waliposhiriki kwa mara ya mwisho.
Ndege ya Amol Yadav iliwekwa kwenye maonyesho mwezi mwaka uliopita
Miaka saba iliyopita Amol Yadav alitangaza
kwa familia yake na marafiki kuwa angejenga ndege juu ya nyumba
yao katika mji wa Mumbai India.
Familia na marafiki waliokua wamepigwa na butwa walimuuliza rubani huyo ni vipi angeweza kuishukisha ndege ikikamilika
"Kwa uhakika sijui," aliwajibu.
Bw Yadav ni rubani wa ndege za kutumia injini mbili.
Walijikakamua
kupandisha vifaa vya kuijengea ndege hiyo hadi paa la nyumba ya familia
la ghorofa tano, ikiwemo injini iliyonunuliwa kutoka ng'ambo ya zaidi
ya kilo 180.
Ilipokuwa ikijengwa juu ya paa la nyumba
Mwezi Februari mwaka uliopita, ndege hiyo ya injini moja yenye nafasi ya watu 6 ilikuwa imekamilika.
Kulingana na Bwa Yadavm, ndege hiyo ndiyo ya kwanza kujengewa nyumbani nchini India.
Anasema
kuwa injini hiyo ina nguvu za kuiwezesha ndege hiyo kupaa umbali wa
futi 13,000 na tanki lake linaweza kubeba mafuta ya kuiwezesha ndege
hiyo kusafiri umbali wa kilomita 2000 kwa kasi ya kilomita 342 kwa saa.
Serikali ilikuwa imeandaa maonyesho ya vifaa vilivyotengenezwa chini India mji Mumbai.
Ikipelekwa kufanyiwa majaribio
Wakati Yadav aliomba ruhusa kutoka kwa waandalizi
kuonyesha ndege yake, walikataa wakisema kuwa hakukuwa na nafasi ya
kutosha. Ilibidi ndugu wake wang'ang'a kutafuta nasafi.
"Kwa hivyo
tuliamua kuobomoa ndege hiyo ili tuishukishe kwa sehemu tofauti na
tuipeleke kwa maonyesho kwa lazima na kuionyeha kwa dunia, Bw Yadav
alisema.
Waliibomoa ndege na kutenganisha injini, mkia na mabawa na kuishukisha kwa kutumia kreni.
Sehemu hizo ziliwekwa kwenye lori na kusafirishwa huku sehemu nyingine ikivurutwa na gari ndogo umbali wa kilomita 25.
Ndege hiyo kwa sasa imeegeshwa katika uwanja wa ndege ya Mumbai
Waliruhusiwa kuingia kwa maonyesho ambapo yeye na mafundi wake waliiunganisha ndege hiyo kwa muda wa saa tatu.
Wakati maonyesho yalianza ndege hiyo iliwavutia watu wengi.
Gazeti
moja liliandika taarifa hiyo hali iliyochangia wageni wengi kufika
akiwemo waziri wa safari za ndege wa India na wafanyabiashara.
Bwana Yadav sasa anasema kuwa yuko tayari kujenga ndege ya kwanza kabisa kujengwa India.
Wawekezaji
wameonyesha moyo wa kuwekeza na serikali ya BJP imeahidi kumpa ekari
157 za ardhi za kujenga kiwanda cha kuunda ndege za kubeba abiria 19.
Bw Yadav saa anajenga ndege yaabiria 19 juu ya nyumba
Mahakama kuu ya Dar es salaam imemhukumu muigizaji
wa filamu, Elizabeth Michael, maarufu kama 'Lulu', kifungo cha miaka
miwili baada ya kumtia hatiani kwa kuua bila kukusudia msanii mwenzake
marehemu Steven Kanumba.
Marehemu Steven Kanumba alifariki majira
ya saa nane usiku,mnamo mwaka 2012 baada ya kutokea mzozo kati yake na Elizabeth Michael ambaye inaaminika kuwa walikuwa na uhusiano wa
Kimapenzi.
Picha za tembo wawili wanaoonekana wakiutoroka umati
wa watu uliowachoma moto imeshinda tuzo kuu katika shindano la picha za
wanyama pori.
Picha za tembo
wawili wanaoonekana wakiutoroka umati wa watu uliowachoma moto imeshinda
tuzo kuu katika shindano la picha za wanyama pori.
Picha ya
Biplab Hazra inaonyesha tembo mtoto akichomeka moto huku yeye na tembo
mkubwa wakitoroka kwa kuhofia maisha yao mashariki mwa India.
Akitangaza tuzo hiyo, jarida la Sancuary lilisema kwamba unyanyansaji wa aina hii unafanyika mara kwa mara.
Picha hiyo ilichukuliwa magharibi mwa Bengal ambako migogoro kati ya wanyama na binaadamu imekithiri.
Haijulikani
ni nini haswa kilichotokea kwa wanyama hao katika picha hiyo ilioshinda
tuzo ambayo ilipigwa katika wilaya ya Bankura. Picha ya Tembo waliochomwa moto yashinda tuzo
Wilaya hiyo imekuwa ikigonga vichwa vya habari kwa vifo vya binadamu vinavyotokana na mzozo na tembo.
Ujumbe
huo ulisema ''Umati wa wanaume waliokuwa wakiwazomea tembo hao ulikuwa
ukiwachoma'' wakati Biplab Hazra alipopiga picha hiyo.
Anakumbuka kelele za ndovu hao walipokuwa wakitoroka.
''Kwa wanyama hao wazuri ,wanaowavutia Jamii sasa wako katika hali ya mbaya'', aliongezea.
Picha hiyo imevutia wengi katika mitandao ya kijamii.
Mainak
Mazumdar anayeishi Bankura, alisema kuwa wanakijiji ni wa kulaumiwa kwa
kuharibu mazingira ya wanyama pori na kwamba tembo wamekuwa
wakinyanyaswa ma kuteswa.
Lakini alisema tembo wamewatesa wanadamu kwa kuharibu mimea yao, mashamba na kuwaua wato wasio na hatia