Ni simulizi ya
ulaji njama ambayo bila shaka imevuma zaidi kushinda njama nyingine
zote. Ni wachache sana ambao hawajawahi kusikia kuwahusu Illuminati.
Huaminika
kuwa kundi maalum la watu ambao hudhibiti masuala na uongozi wa dunia,
na inasadikika kuwa hufanya shughuli zao kisiri kudhibiti kila kitu na
kuunda Utawala Mpya wa Dunia.Kwa wengine, wamehusishwa na utajiri wa ghafla ambao si wa kawaida.
Ukitajirika haraka, kunao bila shaka watakaodai kwamba umejiunga na Illuminati.
Je, kuna ukweli wowote kuhusu wasiwasi huu? Kuna kundi la watu wanaofanya vikao vya siri kupanga njama za kuitawala dunia na pia kjifaidi wenyewe kwa pesa na utajiri?
Simulizi hizi na umaarufu wa illuminati zina ukweli wowote?
Wasiwasi huu kuhusu kundi linalopanga njama ya kuweka utawala mpya duniani ulianza miaka ya 1960, sana kutokana na ubunifu wa watu fulani.
Kuenea kwa habari hizo kunatoa viashiria fulani kuhusu jinsi binadamu walivyo tayari kuamini mambo wanayoyasikia au kuyasoma, kwa urahisi sana. Aidha, kunaweza kutoa funzo kuu kuhusu taarifa na habari za uongo ambazo zinaenezwa mtandaoni siku hizi.









