Polisi nchini
Italia wamemkamata mwanamume ambaye anadaiwa kutumia sumu ya kuua panya
kuwaua watu wa familia yake kwa sababu hawakuwa "wasafi".
Mattia Del Zotto, 27, analaumiwa kwa kuweka sumu kwenye chakula cha babu na nyanya yake na cha shangazi ambao walifarikiWatu wengine watano katika familia wanaendelea kupata matibabu hospitalini.
Bw. Del Zotto alikamatwa eneo la Mozna karibu na Milan baada polisi kupata risiti kwenye kompiuta yake.
Baada ya kukamatwa alikiri kuwa alitaka kuwaadhibu watu wasio wasafi.
Mama yake aliwaambia wachunguzi kuwa hivi karibuni alikuwa amejiunga na dhehebu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni