Jumanne, 26 Mei 2015

MAANDALIZI YA UZINDUZI WA MANJANO FOUNDATION YAKAMILIKA

Wasichana waliochaguliwa kunufaika na Mpango huo wakiwa Katika Picha ya Pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama  Shekha Nasser  

Shear Illusions inasherehekea mwongo mmoja wa urembo nchini Tanzania kwa kuzindua vipodozi vyake ijulikanayo kama LuvTouch Manjano!
Uzinduzi huu utafanyika tarehe 31 Mei 2015 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee VIP Hall. Shamrashamra hizi pia itatoa fursa kwa kuendeleza mtandao wa kibiashara kwa kina mama na pia mada mbali mbali ya jinsi ya kujikwamua kimaisha itatolewa. Bila ya kusahau mafunzo ya jinsi ya kutumia vipodozi.
Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda na mtoa mada mkuu atakuwa ni Balozi Mwanaidi Majaar.

JOTO LAUA 800 INDIA

Raia mmoja wa India akipoozesha mwili wake kwenye bomba kutokana na wimbi la joto linalovuma nchini India.
Takriban watu 800 wamekufa kutokana na wimbi la joto linalovuma nchini India.
Watafiti wamesajili kiwango cha juu mno cha nyuzijoto 500C katika maeneo mengi nchini humo.
Vifo vingi zaidi vimeripotiwa katika majimbo ya kusini ya Telangana na Andhra Pradesh, ambapo watu 140 wamepoteza maisha yao kuanzia jumamosi wimbi hilo la joto lilipotokea.
Mji wa Allahabad ulioko Uttar Pradesh ulisajili vipimo vya nyuzijoto 480C huku wakaazi wa mji mkuu wa India New Delhi ukistahimili kiwango cha nyuzijoto 440C .

POLISI WAKABILIANA NA AL SHAABAB







Wanamgambo wa Al Sbaab wamekuwa wakitishia hali ya usalama nchini Kenya

Askari mmoja ameripotiwa kujeruhiwa baada ya kuwepo kwa mapambano makali kati ya Polisi na Wanamgambo wa Al Shabaab Kaskazini Mashariki mwa Kenya
Wizara ya usalama wa Taifa nchini Kenya imethibitisha kuwa askari mmoja amejeruhiwa wakati wa shambulizi la Wanamgambo wa al shabaab katika kijiji cha Yumbis mjini Garissa, Kaskazini Mashariki mwa Kenya. Msemaji wa wizara hiyo Mwenda Njoka ameiambia BBC kuwa kulikuwa na makabiliano makali kati ya Polisi na wapiganaji hao.
Viongozi katika eneo hilo wamesema Magari manne ya Polisi yamechomwa moto na wanamgambo. Polisi wameiambia BBC kuwa wamepeleka kikosi kuimarisha hali ya usalama.
Taarifa za awali zilieleza kuwa askari kadhaa wanahofiwa kufa kwenye kwenye shambulio la usiku wa jumatatu.
Wakati huo huo al shabaab wamedai kuhusika katika shambulio hilo wakidai kuwa wamewaua Polisi 20, lakini vyombo vya usalama vimesema madai hayo ni Propaganda.
Siku ya jumatatu Polisi watatu walijeruhiwa baada ya Gari lao kukanyaga Bomu la kutegwa ardhini.
Kikosi cha askari 20 kilifika katika eneo hilo kuwasaidia waliojeruhiwa wanaoelezwa kushambuliwa na Al Shabaab.
Al shabaab wamekiri kuhusika katika shambulio hilo na kuchoma magari mjini Garissa. Msemaji wa kundi hilo Shaykh Abdiasis Abu Mus’ab amesema shambulio hilo limefanywa na kikosi maalum kiitwacho ‘mujahidin’.
Mus’ab amesema shambulio lilikuwa la “mafanikio” na kudai kuwa hasara waliyoipata askari wa Kenya ni kubwa.

GARI ZA KIVITA ZABEBA MAHARUSI

Wakala wa harusi wanadai magari ya kifahari (limo) hayana shamrashamra
Wakala wa maandalizi ya Harusi mjini Moscow wamewakodishia magari ya kivita( Deraya) maharusi wapya ili yawasindikize kwenda kwenye sherehe yao badala ya kukodi gari ya kifahari aina ya limo kwa madai kuwa hayaleti shamrashamra katika sherehe.
Wakati magari hayo ya Deraya ni kawaida kuonekana katika mitaa ya Moscow kwa ajili ya gwaride za kijeshi, kwani hukodiwa katika safari za migahawa au ofisi au wakati wa kampeni kwa thamani ya dola 2,000 au Euro1,300.
Meneja wa wakala hao ameiambia Televisheni ya Urusi, NTV kuwa kila kitu hutegemea usajili,Kama wewe usajili wako ni kuendesha gari kando ya Barabara ya Moscow au katikati basi gharama zinatofautiana;kodi ya gari ya Deraya itakuwa ghali zaidi, na kama unataka kutumia pesa kidogo basi inabidi kuepuka kutumia barabara za katikati ya jiji kabisa na kutoka nje kidogo. Afisa wa polisi aliiambia Redio ya Ekho Moskvy kwamba kazi ya magari ya Deraya ni kuchukua vifaa vikubwa na kwa hiyo kuna haja ya ruhusa maalum kutoka mamlaka husika na uratibu wa Polisi.

MOTO WAZUKA KATIKA GHALA LA KUHIFADHIA BIDHAA DAR

MOTO huu umezuka leo asubuhi katika ghala la kuhifadhia bidhaa mbalimbali maeneo ya barabara ya Pugu jijini Dar es Salaam. (Picha kwa hisani ya Times FM)

TUMETOKA MBALI: MKUBWA ANAKUWA MDOGO NA MDOGO ANAKUWA MKUBWA

 
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Kikwete akiwa na Katibu wa CCM Mh Abdulrahaman Kinana

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YATANGAZA RATIBA YA UCHAGUZI MKUU 2015


VITU 5 VILIVYOPIGA MARUKUA DUNIANI LAKINI TZ RUKSA

Nimekusanya list ya vitu 5 ambavyo kwa nchi za wenzetu kama Marekani, Ujerumani, Hispania, Ufaransa na Bangladesh pamoja na sehemu nyingine duniani ni vitu ambavyo kisheria vimepigwa marufuku lakini kwa huku kwetu ni halali kabisa kutumika.

Hii hapa list ya vitu hivyo.
1. Baby Walker

Mwaka 2004 Canada ilipitisha sheria ya kukataza Baby walkers ndani ya nchi hiyo wakidai kwamba mtoto akitumia baby walker anachelewe kutembea na pia kudumaza akili. Mtu yoyote atakayekutwa anamiliki au ananunua kifaa hicho faini ni dola 100,000 au kifungo cha miezi 6 jela.
2. Tomato Sauce #HeinzKetchup

Kama ulihisi Tomato Sauce zote ni ruksa kila sehemu basi jibu ni hapana. Mwaka 2011 tomato sauce ya ‘HEINZ TOMATO KETCHUP’ ilikatazwa kutumika kwenye Kanteen za shule Ufaransa na pia ilikatazwa kusafirishwa kwa baadhi ya nchi za Ulaya.

3. Mifuko ya Rambo.

Nchi ya kwanza kukataza mifuko ya rambo kutumika ni Bangladesh kwa sheria iliyopitishwa huko mwaka 2002.. California nako walipitisha Sheria hiyo mwaka 2012-13 na mpaka sasa hakuna sehemu utaenda California alafu ukawekewa kitu kwenye mfuko wa rambo.
4. Big g

Mwaka 1992 Singapore ilipitisha sheria iliyokataza kuuza ama kusafirisha big g kwa nchi yoyote duniani, ila big g zitengenezwe kwa ajili ya kulika na kununuliwa na raia wa Singapore tu. Baada ya miaka 12 yalifanyika mabadiliko na kuruhusu watu wa Singapore kununua big g ambazo hazina sukari yani Sugar-free chewing gums ambazo ni nzuri kwa meno na kinywa cha binadamu. Kwa sasa utaratibu uliopo ukikutwa unatema big g chini au unatafuna ovyo unapigwa faini.

5. Majina ya watoto

Ujerumani na Denmark kisheria hawaruhusiwi kuwapa watoto majina yoyote nje ya majina 7000 ambayo tayari yamepitishwa, ikitokea mtu atapenda kumuita mwanae jina alipendalo basi atatakiwa kuomba kibali maalum kanisani alafu baadae maombi hayo yanawasilishwa Serikalini, jina likipitishwa basi unaruhusiwa kulitumia.

EDWARD LOWASSA AFUNGUKA MAZITO DODOMA LEO


Waziri Mkuu aliejiuzulu Edward Lowassa amesafirisha wahariri wakuu wa vyombo vyote vya habari toka Dar es salaam na kufanya nao mkutano maalum leo nyumbani kwake mjini Dodoma. Katika mkutano huo kwa ufupi Lowassa amesema yafuatayo;
1. Hahusiki lolote na sakata la Richmond na ndio sababu hata kamati ya Mwakyembe haikuona sababu ya kumhoji. Amesisitiza kuwa cheo cha uwaziri mkuu ndio ilikuwa lengo la kamati ya Mwakyembe na spika wa bunge kipindi hicho Samwel Sitta. Amesisitiza hicho sio kikwazo kwake katika kuingia Ikulu kwani sakata la Richmond lilipikwa kumchafua. Amechukua muda mrefu kuzungumzia hili la Richmond na amesema atalisema zaidi Arusha wikiendi hii.

Jumatatu, 25 Mei 2015

UNESCO YASISITIZA UPENDO KWA WATOTO WENYE ALBINISM

DSC_1073
Mdau Semeni Kingaru akimsimamia kula chakula cha mchana mtoto mdogo kuliko wote mwenye albinism aliyeonekana kukosa upendo wa wazazi wake kwa kipindi kirefu na kufarijiwa na ugeni huo uliofika shuleni hapo.
DSC_1101
Mbunge wa viti maalum CCM, anayewakilisha watu wenye ulemavu, Mh. Al shaymaa Kwegyir akibadilishana mawazo na mabinti wa shule ya msingi Mitindo alipowatembelea na Bi. Zulmira Rodrigues.

DSC_1106
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akisaidiana na Mdau Semeni Kingaru kugawa zawadi ya juisi kwa watoto wa shule ya msingi Mitindo.