Alhamisi, 2 Januari 2014

BOMU LAJERUHI WATU SITA MKOANI ARUSHA


Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas.

Askofu mkuu wa kanisa la Katoliki, jimbo kuu la Arusha Josephat Lobulu akitoa pole kwa baadhi ya majeruhi wa bom.

Watu sita wamejeruhiwa na kile kinachodhaniwa ni bom la kurusha eneo la lake tatu USA river wilayani Arumeru mkoani Arusha siku ya mkesha wa mwaka mpya walipokuwa wakitoka kanisani kuelekea majumbani kwao.

Wakizungumza na BERTHA BLOG, kwa nyakati tofauti katika hospitali ya Tengeru iliyopo wilayani Arumeru, baadhi ya majeruhi wa tukio hilo walisema kuwa siku ya mkesha wa kuupokea mwaka 2014 walipokuwa wakitoka kanisani (Kanisa katoliki parokia ya USA river) waliweza kusikia mlio mkubwa wa kitu kama bom la kurusha ndipo baadhi yao walioangukiwa na bom hilo kuweza kujeruhiwa vibaya na kuanguka chini huku wakivuja dam nyingi sehem mbalimbali za mwili.

Walisema kuwa bom hilo lililorushwa na Askari wa jeshi la polisi mkoani Arusha lilikuwa na lengo la kuwatawanya watu waliokuwa wakichoma matairi barabarani katika eneo hil ikiwa kama sehemu ya kusherehekea mwaka 2014.

Kwa upande wake Askofu mkuu wa kanisa la katoliki jimbo kuu la Arusha, Josephat Lobulu akizungumzia tukio hilo alisema kuwa ni tukio la kulaaniwa, hivyo ameliomba jeshi la polisi kushughulikia jambo hilo.

Alisema kuwa amesikitishwa na tukio hilo, lakini yeye kama mtumishi wa Mungu anapaswa kuwaombea wote walioathrika na tukio hil ikizingatiwa wamepatwa na tukio hilo mita chache tu kutoka katika nyumba ya Mungu (Kanisani).

Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas akizungumza na waandishi wa habari, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kulifuatilia kufaham chanzo cha tukio hilo
"Taarifa nimezipata lakini uchunguzi unaendelea kujua chanzo na muhusika sambamba na ukweli wa mlipuko huo ili kujua kama kweli ni bom na ni la aina gani

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni