Jumamosi, 11 Januari 2014

KIKAO CHA RCC MOROGORO CHARIDHIA MKOA KUGAWANYWA

Kikao cha bunge la mkoa wa Morogoro kilichoketi tarehe 10/1/2014 katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Morogoro kiliamua kwa kauli moja kuwa mkoa wa Morogoro ambao ni mkubwa kuliko yote nchini kugawanywa na kuwa mikoa miwili.

 

Sambamba na hili pia mkutano ulikubaliana na ombi la wananchi wa wilaya ya Ulangala  kugawa wilaya ya hiyo kuwa wilaya mbili za Ulanga na Malinyi.

 

Mkoa mpya utaitwa Mkoa wa Kilombero au Ulanga na utakuwa na wilaya za Ulanga, Malinyi, Kilombero na Kilosa. Mkoa mwingine utakuwa ni mkoa wa Morogoro ambao utakuwa na wilaya za Morogoro, Mvomero, Gairo na Morogoro Mjini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni