Alhamisi, 16 Januari 2014

MTU MCHAFU KULIKO WOTE DUNIANI HAJAOGA KWA MIAKA 60

 

Mtu anayeaminika ni mchafu kuliko wote duniani bwana Haji mwenye miaka 80 anaamini kuwa usafi utamletea maradhi. Hii ndio maana hajaoga kwa miaka 60 sasa. Anaishi kwenye kijiji kilichojitenga cha Dejgah, kusini mwa nchi ya Iran kwenye jimbo la Fars.
Haji anachukia sana kugusa maji na wazo la kuoga linamkasirisha sana. Kwa sasa Haji anafanana sana na rangi ya udongo na ikiwa akikaa kinya unaweza kudhani kuwa ni jiwe.
Haji hachukii maji tu ila anachukia chakula kizuri na maji safi ya kunywa. Yeye anapenda chakula kilichotengenezwa kwa nyama ya karunguyeye aliyeoza na anakunywa lita 5 za maji kwa siku ingawa yanawekwa kwenye chombo ya kuwekea oil ambacho kimepiga kutu. Anavuta kiko ambacho kimewekwa samadi badala ya tumbaku. Hakati nywele ila anazichoma moto
Amou-Haji2
Photo: IRNA
Haji hana nyumba bali anaishi shimoni kama kaburi. Wenyeji wanamuita Amou Haji na maana ya Amou ni aina ya mtu mzee.
Amou-Haji
Photo: IRNA


Sources: The Nation, Tehran Times

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni