Jumatatu, 6 Januari 2014

Prof Maghembe atembelea mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi,(MUWSA


)

Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini
Moshi,MUWSA,Injinia Cyprian Luhemeja akimsindkiza waziri wa maji
Jumanne Maghembe kujionea shuguli za uchimbaji wa kisima katika eneo
la tanki la maji la Kilimanjaro.
Waziri Maghembe akitoa maelekezo kutoka kwa mkandarasi anaye chimba
kisima katika eneoo la tanki la maji la Kilimanjaro.
Mitambo ya kuchimbia visima ya kampuni ya DDCA ikiendelea na shughuli
za uchimbaji katika eneo la tanki la maji la Kilimanjaro.
Chanzo cha maji cha Coffee Curing ambacho kimefanyiwa ukarabati kwa
ajili ya kusaidia ongezeko la maji kwa watu wa kata ya Bomambuzi.
Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi,Injinia
Cyprian Luhemeja akitoa maelezo ya kwa waziri wa maji Prof Jumanne
Maghembe katika tanki la maji la Kilimanjaro.

Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi,Injinia
Cyprian Luhemeja akisoma taarifa mbele ya waziri wa maji Prof Jumanne
Maghembe.
Maofisa wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi wakifuatilia
maelezo ya waziri Maghembe alipotembelea mamlaka hiyo kujionea
utekelezaji wa mipango iliyojiwekea ndani ya siku 180.
Waziri wa maji Prof Jumanne Maghembe akizungumza na watendaji wa
mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi,(hawapo pichani) muda
mfupi baada ya kutembelea tanki la maji la Kilimanjaro na chanzo cha
maji cha Coffee Curing.
Mwenyekiti bodi ya wakurugenzi ya mamlaka ya maji safi na maji taka
mjini Moshi,Shally Raymond akitoa neno la shukrani kwa waziri wa maji
Prof Maghembe alipotembelea mamlaka hiyo.

======== ======== ==========
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.

TAASISI za serikali nchini zikiwemo hosptali ,majeshi ya Polisi na
Magereza zimetajwa kuwa ndio wadaiwa wakubwa wa Ankara za maji ambazo hadi sasa zinafikia kiasi cha zaidi ya shilingi ya sh bilioni 10
jambo linalosababisha baadhi ya mamlaka za maji kupata changamoto
kutekelezaji mipango yake

Waziri wa maji, Profesa Jumanne Maghembe, alisema hayo akijibu baadhi
ya maswali kutoka kwa waandishi wa habari sanjari mwenyekiti wa bodi
ya mamlaka ya majisafi na majitaka mjini Moshi(MUWSA) baada ya
kutembelea tanki la maji Kilimanjaro na chanzo coffe curing mjini
hapa.

Tayari deni hilo limewasilishwa serikalini kwa utaratibu maalum na
kwamba mipango ni kuona kwamba kila fedha zinapopatikana zinalipwa ili
kupunguza ama kumaliza kabisa deni hilo.

“Madeni haya ni kero,lakini tangu tumeyawasilisha serikalini, yapo
mashiriki ambayo tayari yameanza kulipwa fedha hizo,sielewi ni kwanini
MUWSA haijalipwa….nadhani baada ya mkutano wetu huu watasikia na
kuanza kuyalipa kwa kasi Zaidi”alisema Maghembe.

Hata hivyo,Profesa Maghembe,alipongeza juhudi za mamlaka katika
kuongeza vyanzo vya maji na kuondokana na mgawo uliokuwepo awali huku
akitaka maeneo ya Majengo,Bomambuzi, Kiborlon na maeneo mengine ya
pembezoni kupewa kipaumbele Zaidi.

Awali katika swali lake la msingi,mwenyekiti wa bodi ya MUWSA, Shally
Raymond, alitaka kufahamu juhudi za serikali katika kulipa madeni ya
Ankara za maji kwani kutolipwa kwa fedha hizo ni kikwazo katika
utekelezaji wa baadhi ya shughuli za mamlaka hiyo.

Mapema katika taarifa yake kwa waziri Maghembe,mkurugenzi wa mamlaka hiyo,mhandidsi Cyprian Luhemeja alisema wamefanikiwa kuongeza chanzo cha coffe curing chenye lita za ujazo wa 1500 huku juhudi za kuchimba kisima katika tanki la Kilimanjaro kitakachokuwa na lita za ujazo 1800 kwa siku zikiendelea.

Alisema mamlaka ilijipa muda wa siku 180 kutekeleza mipango yake
ambapo walikusudia kukarabati miundombinu na kuondoa mtandao mbovu
wenye urefu wa Km 85 lakini hadi kufikia juzi mchakato wa kuondoa Km
24 umekamilika ambapo vifaa vimeshanunuliwa.


Kuhusu upotevu wa maji,mkurugenzi huyo alisema kwa kipindi cha Juni
2013 kulikuwa na upotevu wa mai wa asilimia 38 lakini hadi kufikia
disemba mwaka 2013 kiwango hicho kilishuka hadi kufikia asilimia 24 na
mipango ni kufikia asilimia 9 ifikapo Juni 2014

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni