Madaktari katika hospitali kubwa zaidi ya umma nchini
Kenya,Kenyatta, wamefanikiwa kutoa risasi iliyokuwa imekwama katika ubongo wa
mtoto Satrine Osinya mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.
Risasi hiyo iliyomuingia mtoto Satrine kichwani ndiyo iliyomuua mamake.
Mamake Satrine alikuwa amempakata mtoto wake ili kumlinda kutokana na magaidi
waliovamia kanisa walimokuwa wiki moja iliyopita katika mtaa wa Likoni mjini
Mombasa.
Lakini walimpiga risasi mama huyo na kumuua papo hapo huku risasi iliyomuua
mama huyo ikiingia kichwani mwa Satrine na kukwama kwenye ubongo wake.
Satrine alipelekwa Nairobi kwa matibabu maalum kutoka Mombasa kutokana na
ukosefu wa wataalamu wa upasuaji wa ubongo mjini humo.
Shughuli ya kuondoa risasi hiyo ilichukua saa tatu na ilifanywa na madaktari
watatu wakiongozwa Daktari Mwangi Gichuru ambaye ni mkuu wa kitengo cha upasuaji
wa neva katika hospitali hiyo.
Matoto Satrine yuko salama na daktari Mwangi anasema hawakupata matatizo
walipokuwa wanafanya upasuaji huo(TK)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni