200 wakamatwa baada ya shambulizi Kenya
Watu 25 walijeruhiwa vibaya katika shambulizi hilo lililotokea
Jumatatu usiku
Polisi nchini Kenya wanasema kuwa wamewakamata zaidi ya watu
200 kufuatia mashambulizi ya hapo jana Jijini Nairobi ambapo takriban watu sita
waliuawa.
Wengine 25 walijeruhiwa katika mashambulizi hayo matatu yaliyotokea kwa
wakati mmoja katika mtaa wa Eastleigh ambapo raia wengi wa kisomali wanaishi na
kufanya kazi.
Polisi wanasema kuwa milipuko hiyo iliyotokea katika mikahawa miwili midogo
huenda ilisababishwa na magurunedi pamoja na mabomu la kujitengezea.
Kumekuwa na mashambulizi kadhaa mjini Nairobi pamoja na mjini Mombasa katika
miezi ya hivi karibuni, ambapo polisi wanawalaumu waislamu wenye itikadi kali (TK).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni