Jumanne, 1 Aprili 2014

WAKAMATWA NA MENO 53 YA TEMBO NA SMG

Lazaro-Nyarandu-April1-2014_1c29c.jpg
Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu.

Kikosi dhidi ya Ujangili Kanda ya Kati kwa kushirikiana na Kikosi Kazi Maalum, kimewakamata watu sita kwa tuhuma za kukutwa na silaha ya kivita aina ya Sub Machine Gun (SMG), magazini tatu na meno ya tembo 53 yenye jumla ya kilo 169.7.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, aliwaeleza waandishi wa habari jijini hapa jana kuwa wathumiwa hao walikamatwa usiku wa kuamkia jana katika kijiji cha Kiombo, Wilaya ya Manyoni, mkoani Singida.

Idadi hiyo ya meno ambayo thamani yake bado haijajulikana, inaonyesha kuwa jumla ya tembo 26 wameuawa na majangili katika maeneo ya Pori la Akiba la Rungwa na Kizigo.

"Msako zaidi unaendelea kuwakamata watu wote waliohusika na mtandao wa mauaji ya tembo hao 26," alisema.

Hata hivyo, Waziri Nyalandu alisema majina ya watuhumiwa hao wa ujangili ambao wote ni Watanzania, yatatajwa baadaye, lakini alisema wanatarajiwa kufikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo (TK).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni