ZITAMBUE FAIDA 10 ZA ULAJI WA UKWAJU NA HIZI NDIZO FAIDA ZAKE KATIKA MWILI WA BINADAMU.
Hizi Ndiyo Faida Kumi (10) Za Kula Ukwaju!
Unatakiwa ujaribu kuweka ukwaju karibu katika kila mlo wako kwa
kila siku kwasababu ukwaju una faida nyingi kiafya ambazo hakika zitakufanya uwe
na afya njema au kukuimarisha afya yako kiujumla
Watu waishio bara la Asia,
Carribian na America ya kusini wanajua kuwa kula ukwaju maana yake ni Afya
Njema.
Ukwaju unaoliwaa katika maeneo haya maeneo hayo una faida
nyingi kwa watu wanaoula.
Kwa hiyo siku nyingine unapoenda kufanya manunuzi ya
vyakula
hakikisha unanunua na ukwaju. Ukwaju ni zao la rangi ya
kahawia
ambalo limefungwa na kasha gumu. Ndani ya kasha hilo kuna vifundo
vilaini ambavyo ndani yake kuna mbegu nyeusi.
Vifundo hivi ndiyo ambavyo
watu wanakula ili kupata virutubisho na
faida za kiafya za ukwaju.
Ukwaju
una ladha faluni ya uchachu
ukiwa bado mchanga, lakini kadiri unavyozidi
kukomaa unakuwa na ladha tamu. Ingawa ukwaju unakuwa na utamu
kadiri
unavyokuwa na kukomaa, kiujumla ukwaju ni mchachu.
Katika nchi
kama Jamaica, Mexico, Aruba na India, ukwaju
unachanganjwa na sukari na
kuuzwa kama pipi katika mitaa na
madukani. Kula ukwajua au bidhaa zitokanazo
na ukwaju kuna faida sana. Ukwaju umejaa Vitamini, fiber, potassium, magnesium
na virutubisho vingine muhimu kwa afya njema.
Lakini kati ya faida
zingine nyingi za virutubisho na kiafya za
ukwaju, kuna kadhaa ambazo ni za
muhimu zaidi, na ni kama
zifuatazo:
1. Ukwaju chanzo kizuri sana cha
antioxidants ambazo zinasaidia kupigana na saratani. Ukwaju una carotenes,
Vitamini C, flavanoids na vitamin B zote.
2. Ukwaju unakuepeusha na
ukosefu wa Vitamini C.
3. Ukwaju unasaidia kupunguza homa na kukupa
ulinzi dhidi ya
mafua.
4. Ukwaju unakusaidia kuyeyusha chakula
tumboni.
5. Ukwaju unakusaidia kutibu matatizo ya nyongo.
6.
Juisi ya ukwaju hutumika kama kitu cha kustarehesha mwili.
7. Ukwaju
unapunguza cholesterol mwilini.
8. Ukwaju unasaidia kuwa na moyo wenye
afya njema.
9. Ukwaju ukiunywa unasaidia kupooza koo.
10. Ukwaju
ukiupaka kwenye ngozi unasaidia kutibu uvimbe
Kwa Tanzania ukwaju unapatikana
kwenye masoko
karibu yote.
Manyandahealthy inakushauri
kutengeneza juisi ya ukwaju nyumbani kwako na weka sukari kidogo na juisi hiyo
iwe sehemu ya chakula chako. Kama wewe unapenda kula hotelini au kwenye
vioski basi agizo juisi ya ukwaju ikusaidi kushushia
chakula.
http://www.manyandahealthy.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni