Uchaguzi wa Malawi ulikumbwa na visa vingi vya wizi wa kura
pamoja na udukuzi wa mitambo iliyokuwa inatumiwa kujumlisha kura. Haya ni madai
ya Rais Joyce Banda.
Rais Joyce Banda ametaka kura hizo kuhesabiwa upya bila ya kutumia mitambo ya
elektroniki ya kuhesabu kura.
Bi Banda alikumbwa na ushindani mkali katika uchaguzi huo uliofanyika siku ya
Jumanne kutoka kwa wagombea watatu akiwemo, waziri wa zamani wa mambo ya nje
Peter Mutharika.
'Waziri ajiua'Mapema Alhamisi naibu waziri wa serikali za mitaa wa Malawi alijipiga risasi na kujiua nyumbani kwake mjini Lilongwe.
Godfrey Kamanya alikuwa anagombea kutetea kiti chake cha ubunge katika jimbo la Nzonzi Kusini.
Alijiua alfajiri ya leo katika mojawapo ya vyumba vya nyumba yake iliyopo Area Ten mjini Lilongwe.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali kuu ya Kamuzu mjini humo, na jeshi la polisi litatoa taarifa rasmi ya kifo hicho baada kukamilisha uchunguzi.
Haijajulikana sababu za Kamanya kujiua japokuwa ameacha barua ya maelezo ambayo polisi wataitoa baadae.
Matokeo ya kura bado hayajatangazwa rasmi katika kile kinachosemekana kuwa uchaguzi wenye ushindani mkali sana.
Afisa mkuu wa uchaguzi, amesema kuwa mfumo wa elektroniki umeharibika na maafisa wanatuma matokeo kwa njia ya barua pepe (TK)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni