Meriam mwenyewe alilelewa na mama yake ambaye ni mkristo na kusema kuwa hajawahi kuwa muislamu. Pistelli Naibu waziri wa mambo ya nje wa Italia, aliweka picha yake na Meriam kwenye ukurasa wake wa facebook akisema kuwa wanaelekea kutua mjini Roma.
Mume wa Meriam Daniel Wani, ni mkristo, ana asili ya Sudani kusini na ana uraia wa Marekani.
Mtoto wa Meriam, Maya alizaliwa gerezani mwezi May, muda mfupi baada ya kuhukumiwa kunyongwa hatua iliyosababisha hasira na malalamiko dunia nzima.
Aliachwa huru mwezi Juni baada ya kuwepo kwa mashinikizo lakini alikamatwa tena na alipoacchiwa tena akakimbilia ubalozi wa Marekani mjini Khartoum (TK).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni