TASNIA YA MUZIKI WA IJNILI YAPATA PIGO TENA
Muimbaji Orida Njole enzi za uhai wake
Zikiwa ni takribani wiki tatu tangu
tasnia ya muziki wa injili nchini kumpoteza mmoja wa waimbaji wake marehemu
mchungaji Debora Saidi, taarifa za kifo cha mwimbaji muziki wa injili Orida
Njole zinaeleza kuwa amefariki dunia mchana wa jana hospitali ya Temeke
jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Orida ambaye mpaka umauti unamfika Julai 13 mwaka
huu ilikuwa bado haijajulikana nini hasa kinamsumbua lakini alikuwa ameishiwa
damu sana, mpaka umauti unamkuta alikuwa anatamba na album yake iitwayo 'Duniani
tu wapitaji'.
Bwana alitoa na
Bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni