UNYAMA MKUBWA: BINTI WA MIAKA 16 ACHINJWA SINGIDA
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela
WATU wasiojulikana wilayani
Manyoni wamemchinja mithili ya kuku binti mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa
miaka 16.
Diwani
wa Kata ya Manyoni Mjini, Hamis Masabuni alisema tukio hilo lilitokea juzi
asubuhi katika eneo la Mitoo kwenye mashamba ya Magereza, Uwanja wa Ndege wa
zamani.
Alisema siku ya tukio, yeye alipata taarifa ya simu kutoka kwa
raia wema hivyo ikambidi aende huko kushuhudia kulikoni na mara alipofika eneo
hilo alikuta mwili wa marehemu ukiwa umelala chini na kuchinjwa mithili ya kuku.
Diwani huyo amelitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina juu ya
tukio hilo ili kubaini wauaji wa binti huyo ili hatua za kisheria ziweze
kuchukuliwa dhidi yao.
Muuguzi wa zamu katika hospitali ya wilaya ya
Manyoni, Getruda Njughuda amekiri kuupokea mwili wa binti huyo.
Naye
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela alisema kuwa polisi
inaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo.HABARILEO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni