Jumatano, 6 Agosti 2014

BODABODA MORO WAVAMIA KITUO CHA POLISI NA KUMTOROSHA MAHABUSU

Madereva wa pikipiki wamevamia kituo cha polisi cha Mvuha wilaya ya Morogoro kwa kupiga mawe na kumjeruhi askari mmoja na kisha kumtorosha mtuhumiwa aliekuwa anashikiliwa kwa makosa ya kubebe abiria watatu katika pikipiki moja.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul akizungumza na vyombo vya habari amesema madereva hao walikua wakishinikiza mwenzao kuachiliwa huru ambapo kabla ya tukio madereva wa pikipiki walifanya mgomo kisha kuandamana ambapo alivamia kituo cha polisi na kupiga mawe na kumjeruhi askari mmoja na kufanikiwa kumtorosha mtuhumiwa ambapo jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata watu 18 wanaosadikiwa kuhusika na tukio hilo na watafikishwa mahakamani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni