ALFONSO DHLAKAMA AREJEA MSUMBIJI
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Renamo cha nchini
Msumbiji,Alfonso Dhlakama, ameonekana hadharani katika mji mkuu wa nchi
hiyo,Maputo, baada ya kuwa mafichoni zaidi ya miaka miwili.
Wanachama wa Renamo walionekana katika viwanja vya ndege vya Maputo kumpokea
kiongozi wao, wakiwa na bashasha na nderemo kutokana na kumwona kiongozi wao
hadharani.
Alfonso aliwasili Mjini Maputo akiwa ameambatana na mabalozi kadhaa wanao
wakilisha nchi zao Mozambique,ili kumhakikishia usalama wake,ujio wa Alfonso
umekuja mwezi mmoja tu baada ya kusaini hati ya amani kumaliza harakati za
vikundi vya wanamgambo wa Renamo.
Alfonso anatarajiwa kuingia katika kinyang'anyiro cha kugombea nafasi ya
uraisi katika uchaguzi unaotegemewa mwezi ujao
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni