Jumanne, 23 Septemba 2014

BARCELONA YAFANYA MAUAJI



















Timu ya Barcelona imeipa kipigo cha mbwa mwizi timu ya Levante kwa kuigagadua mabao 5 - 0 katika mchezo wa La liga.
Lionel Messi Barcelona
Lionel Messi na Neymar walishangilia goli.

Goli la kwanza lilitokana na Messi aliyempa pande Neymar ambaye alifunga goli katika dakika ya 34. Goli la pili lilitokana na Messi pia ambaye alirusha mpira na kumkuta Ivan Rakitic ambaye alipiga mpira mrefu na kufunga goli la pili hivyo hadi mapumziko Barcelona 2-0.

Dakika ya 57 messi pia aliondoka na mpira akampa pande Ramirez ambaye alifunga goli la 3.

Goli la nne lilifungwa na Pedro katika dakika ya 64 na Messi akahitimisha karamu ya magoli kwa goli la dakika ya 77.







Hakuna maoni:

Chapisha Maoni