Wapiganaji wa dola ya Kiislam IS wamesambaza picha za video
katika mitandao kwa lengo la kuonyesha kuchinjwa kwa mwandishi wa habari raia
Marekani Steven Sotloff ambaye ni mmoja wa mateka wanaoshikiliwa na wapiganaji
hao.
Mwandishi huyo Sotloff, mwenye umri wa miaka 31 ambaye alitekwa na wapiganaji
hao mwezi August mwaka jana.
Mwezi uliopita Sotloff alionekana mwishoni katika picha za video
zilizoonyeshwa kuhusiana na kuchinjwa kwa mwandishi mwingine wa Marekani James
Foley.
Wapiganaji hao wa katika picha hizo pia wameonekana wakimtishia kumuua mateka
mwingine anayedhaniwa kuwa ni raia wa Uingereza.
Baada ya mauaji ya mwandishi wa awali Foley, mama mzazi wa mwandiashi wa
Sotloff alitoa ombi maalumu kwa kiongozi wa wanajeshi hao Abu Bakr al-Baghdadi
kutomuua mtoto wake.
Msemaji wa Ikulu ya White House Josh Earnest amesema kuwa maofisa wa Marekani
wanaendelea na uchunguzi wa ripoti hiyo.
Marekani hivi karibuni ilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya IS nchini
Iraq.
Mwandishi wa masuala ya usalama wa BBC Frank Gardner amesema hatua hiyo ya
wapiganaji wa IS ni kulipa kisasi kwa Marekani
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni